LYMO: NITAWATUMIKIA IPASAVYO WANANCHI WA KIMANGA.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kimanga kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)Julius Pitter Lymo amesema kuwa atashirikiana Vyema na Wananchi wa kata hiyo katika kutatua changamoto zinazowakabila endapo watampa ridhaa ya kuwa diwani wao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,Mwaka huu.
Amesema hayo leo Agost 15,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi wa kugombea nafasi hiyo kutoka kwa katibu wa CCM Ilala Chief Sylivester Yared.
"Kusema kweli leo nina furaha sana chama Changu kuniamini nakuona kwamba naweza kuwaletea wananchi wa Kimanga Maendeleo,na leo tupo hapa kuchukua barua zetu za uteuzi,hivyo wana Kimanga nawaahidi sito waangusha,nitaitekeleza Vyema Ilani ya Chama Chetu".
Nakuongeza kuwa" Kimanga ina changamoto kubwa ya Miundombinu na mimi katika vipaumbele vyangu namba moja ni Miundombinu,tutajitahidi Kimanga tupate barabara ambazo zita tuunganisha na Kata zingine,vilevile Kimanga ina changamoto ya stendi kwahiyo wana Kimanga wasiwe na wasiwasi,tumejipanga kushirikiana na Mamlaka zingine ili kuondoa kero hizo."
No comments
Post a Comment