Zinazobamba

WAFANYAKAZI WANAWAKE NDC WATOA FARAJA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA MPIJI MAGOHE,WASHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI


Kaimu Mkurugenzi Iadara ya Viwanda vya kuongeza thamani kutoka NDC  ,Esther Mwaigomole

Na Mussa Augustine.

Wakulima wa Sekta ya Mbogamboga wameshauriwa kutumia dawa mpya aina ya "Thurisave 24" inayotengenezwa na Kampuni ya Tanazania Biotech Products Ltd( TBPL) kwani ni salama kwa ikolojia na afya za watumiaji kutokana na kutokua na sumu.

Kiuatilifu hicho ambacho kinatengenezwa na TBPL kampuni tanzu ya Shirikala la Maendeleo la Taifa( NDC)  imeonyesha ufanisi kwenye mazao ya Pamba,Mahindi,Mboga za majani na Matunda lakini pia inaweza kutumika hata kipindi cha mavuno bila kuleta athari kwa mtumiaji na mkulima kupata mavuno mengi bila kuathiri ubora.

 Ushauri huo umetolewa tarehe 7 Machi 2024 na Kaimu Mkurugenzi Iadara ya Viwanda vya kuongeza thamani kutoka NDC  ,Esther Mwaigomole wakati wafanyakazi wanawake wa shirika hilo walipotembelea kikundi cha wakulima wa mbogamboga waliopo Mpiji Magohe jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya Kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani inayofanyika  Machi 8 kila Mwaka Duniani kote.

 Mwaigomole amesema kwamba bidhaa hiyo waliyoitambulisha kwa wakulima hao imezalishwa kwa mara ya kwanza na TBPL  ambapo ikitumika inarutubisha mazingira ,na haina madhara kwa wananchi watakaotumia mboga za majani kwani kiuatilifu hicho huzalishwa kwa kutumia bakteria rafiki wanaopatikana ardhini ,wenye uwezo wa kutoa protini sumu yenye madhara kwa wadudu waharibifu wa mazao katika hatua ya Viwavi ( Caterpillar).

Kwa mujibu wa Mwaigomole kiutalifu hicho cha" Thurisave 24" kimeanza kuzalishwa Desemba 2023 ikiwa lengo ni kuzalisha kiuatilifu ambacho hakina kemikali yenye madhara kwa mazingira na afya ya binadamu nakwamba ipatikane kwa urahisi ndani ya nchi na sio kutegemea kuagiza kutoka nje ya nchi.

  Mmoja wa wafanyakazi wa NDC akitoa mfano wa namna ya kupulizia  kiuatilifu aina ya Thurisave kwenye mbogamboga na mahindi.

" Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani,tumeamua kuja kusaidia kikudi hiki cha wakulima wa mbogamboga hapa Mpiji Magohe,na kutangaza bidhaa yetu mpya ya dawa aina ya Thurisave 24 inayozalishwa na Kampuni tanzu la shirika letu la Maendeleo la Taifa,ambazo niza kibailojia na zinarutubisha mazingira na haina madhara kwa wakulima wenyewe na walaji wa mboga  kwani hazina kemikali" amesisitiza Mwaigomole.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara Mwandamizi kutoka TBPL Jovin Magayana amebainisha kuwa kwa mujibu wa shirikala la afya Duniani ( WHO) asilimia 20 hadi 40 ya mazao yanayolimwa yanaharibika na wadudu dhurifu nakusababisha hasara kubwa kwa wakulima lakini pia Fedha nyingi hutumika kukabiliana na athari hiyo hivyo kiuatilifu hicho cha Thurisave 24 cha TBPL kitasaidia wakulima kupata mazao mengi na yenye ubora.

Hata hivyo baadhi ya wakulima hao akiwemo Sada Simba Maulid na James Mwakitime kwa nyakati tofauti wamesema kwamba bidhaa hiyo itawasaidia kupata mazao mengi na kujikinga na afya zao nakwamba wananchi kwa sasa watakula mboga za majani bila wasiwasi wa afya zao.

Mmoja wa wakulima wa mbogamboga Sada Simba Maulid akipilizia kiuatilifu baada ya kupata maelekezo ya matumizi ya kiuatilifu hicho.

  Baadhi ya Wakulima wa Mogamboga waliojitokeza kuwalaki wafanyakazi wanawake wa NDC (hawapo pichani) ikiwa ni kesherehekea siku ya mwanamke duniani na kupata taarifa ya dawa mpya ya thurisave 24


Hakuna maoni