Kampuni ya Heritage Drinking Water yazindua kituo cha huduma ya Maji Safi na Salama IFM
Na Mussa Augustine. Imeelezwa kuwa serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara inatambua mchango na ubunifu wa biashara unaofanywa na Kampuni ya maji ya Heritage Drinking Water kwa kuanzisha mradi wa kutoka huduma ya maji safi na salama kwa bei nafuu katika maeneo mbalimbali Mkoa wa Dar es Salaam. Afisa Biashara wa Jijini la Ilala Bw.Kefa Gembe(mwenye shati jeupe) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha maji safi na salama katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Hayo yamesemwa leo na Afisa Biashara wa Jijini la Ilala Kefa Gembe wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha maji safi na salama katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo wanafunzi watanufaika kwa kupata maji kwa shilingi mia mbili kwa lita. Aidha Afisa huyo wa Biashara Jiji la Ilala ameihakikishia Kampuni hiyo kuwa Serikali ipo pamoja nayo katika kuhakikisha inaiwekea mazingira bora na rahisi ya utoaji wa huduma ya maji ili iwanufaishe wananchi wengi zaidi na wafike mikoani. “Natambua kuwa maji ni hitaji la msingi kwa mwanadamu, nimevutiwa na kaulimbiu yenu isemayo Heritage Water okoa pesa tunza mazingira , hivyo ninauhakika wananchi na wanafunzi watapata maji safi na salama kwa bei nafuu “ Amesema Bw.Kefa. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Heritage Drinking Water Dkt. Edwinus Lyaya(mwenye suti ya bluu) akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa huduma ya Maji safi na Salama kwa bei nafuu katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Heritage Drinking Water Dkt. Edwinus lyaya ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuikaribisha kampuni hiyo katika taasisi zake ikiwemo shule na vyuo ili itoe huduma ya maji kwa bei nafuu ya shilingi mia mbili kwa lita. Hatahivyo ameziomba Taasisi za Umma na Binafsi kulegeza masharti na kupunguza urasimu ili kuwezesha kampuni hiyo kutoa huduma kwa watanzania ambao bado hawajafikiwa na mradi huo. Aidha amesema kwamba mradi huo unasaidia katika utunzaji mazingira kwa kutumia chupa ngumu za matumizi ya mda mrefu ili kuondoa tatizo la uchafuzi wa mazingira kwa chupa tupu za maji na mifuko ya plastiki. Kampuni ya Heritage Drinking water imefanikiwa kuweka vituo vipatavyo 17 vya kuuza maji kwa bei nafuu katika maeneo mbalimbali Mkoani Dar es Salaam ikiwemo DDC Kariakoo, Dart Gerezani, Chuo cha CBE, Soko la Tandika, Ilala Boma, Chuo cha Ardhi na Ilala sokoni. Vituo vingine ni pamoja na Stendi ya Tegeta Nyuki, Chuo cha MUHAS, Stendi ya Mawasiliano (Simu 2000) Riverside, Mabibo Hostel, Stendi ya Magufuli, Chuo cha IFM, Soko la Samaki Feri pamoja na makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Changanyikeni.
|


1 comment
HERITAGE DRINKING WATER is a fantastic social responsive company that considers quality of service, incomes of people and the general environment of society.
Post a Comment