Filamu zaidi ya 100 kutoka nchi 33 Duniani kuonyeshwa katika Tamasha la ZIFF mwaka 2022.
Na. Vicent Macha
Tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2022 limekuja na mikakati ya kuinua filamu za Kitanzania kufikia katika ubora wa kimataifa, ambapo filamu 101 zitaonyeshwa kutoka nchi 33 duniani.
Mratibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) Prof. Martin Muhando.
Hayo yameelezwa
na Mratibu wa Tamasha Prof.
Martini Muhando wakati akiongea na waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar
es salaam.
Aidha Prof.
Martin amesema kuwa filamu ambazo zinatarajiwa kuonyeshwa kwenye Tamasha la
ZIFF ni kutoka katika mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU), Tanzania, Kenya na Afrika
ya kusini, ambapo itasaidia washiriki kuweza kujifunza tamaduni mbalimbali za
mataifa shiriki.
Ameongeza kuwa ni jambo zuri kuona kwamba kwa nchi kama Iran ambayo ni mara ya
kwanza kushiriki lakini imeweza kuleta filamu Zaidi 660, Na kwa upande wa Bara
la Ulaya pia limeweza kuleta filamu 465.
| Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano kwa umakini. |
Ameendelea kusema
kuwa juni 18 mwaka huu itakuwa siku ya ufunguzi na filamu itakayokuwa ya kwanza
kuonyeshwa inaitwa “Vuta Nkuvute” ambayo imevunja rekodi hapa nchi.
“Tunahisi filamu
hii inayoitwa Vuta Nkuvute itatuinua kidete watanzania na ni filamu ya Afrika Mashariki,
ndio maana imepata nafasi ya kuonyeshwa kwenye tamasha hili la kimataifa (ZIFF)”
Amesema Prof. Martini
Ameongeza
kuwa wakenya licha ya kuwa ni washindani wakubwa n ani watu wenye kuleta
upinzani mkubwa kwa watanzania, lakini pia wamesaidia kuongeza msisimko na
kuleta mafanikio kwenye tamasha la ZIFF na tasnia ya Filamu ya Tanzania.
Amesisitiza kuwa kwa upande wa Afrika ya kusini wamekuwa ni washirika wazuri kwa Tanzania
licha ya harakati za uhuru tu lakini watu kutoka katika taifa hilo wamekuwa
kipaumbele kuzindua na kuleta flamu za katika tamasha la ZIFF.
Lakini pia amewapongeza DW Academy kwani wamekuwa na mchango mkubwa sana katika tamasha hilo na kusema kuwa kwa mwaka wapili mfululizo wamekuwa wakiendesha mafunzo kwa washiriki ya namna ya kuboresha kazi zao ili ziwe na viwango vya kimataifa.
| Baadhi ya wageni waliyofika katika mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia Tamasha la ZIFF 2022. |
No comments
Post a Comment