DC. Jokate apokea msaada wa Pikipiki tano kutoka kampuni ya Hero Motocorp
Na Mussa Augustine.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Jokate Mwegelo ameitaka jamii wilayani humo kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi dhidi ya utoaji wa taarifa za uhalifu kwa ajili ya kuwezesha Jeshi hilo kuchukua hatua na kukomesha vitendo vya uhalifu.
| Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Jokate Mwegelo. |
Mh.Jokate ametoa wito huo wakati akipokea pikipiki tano aina ya Hunter 125cc kutoka kampuni ya Hero Motocorp iloyopo chini ya Kampuni tanzu ya Karemjee Jivaniee Ltd( KJL) kwa ajili yakuliwezesha Jeshi la Polisi Kanda ya Temeke kupambana na vitendo vya uhalifu kwa ufanisi.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Temeke ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo amesema kwamba Wananchi hawawezi Kufanya kazi Kama maeneo yao hayako salama ,nakwamba Wilaya ya Temeke imekithiri kwa vitendo vya uhalifu hususani wizi wakutumia Pikipiki wa kukwapua na kukimbia maarufu Kama Vishandu.
Aidha amendelea kusema kwamba " Mapambano dhidi ya uhalifu ni jukumu letu sote,jamii iendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu na hata Kama ni ndugu yake,hivyo nawapongeza kampuni ya Hero Hunter ambayo ni chata iliyopo chini ya Kampuni ya Toyota kwa kutoa msaada huu wa Pikipiki tano ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu" amesema DC Jokate.
| Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro. |
Awali akizungumza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro amesema kwamba hatua iliyofanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutafuta suluhu ya masuala ya Usalama ni jambo la kupongezwa nakuzitaka kanda zingine za kipolisi ikiwemo Kanda ya Polisi Kinondoni na Ilala kuiga Mfano huo.
" Napenda kuwatahadhalisha askari mtakaotumia pikipiki hizi,msitumie kwa kuomba rushwa,msizitumie kwa ajili yakuwasumbua Wananchi,msizitumie kwa kusindikiza wahalifu ,hivyo zitumike kwa kazi moja tu yakuleta suluhu ya uharifu kwa Wananchi " amesisitiza ACP Muliro .
"Nakuongeza kwamba " Naipongeza kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Temeke kutafuta suluhisho la masuala ya Usalama,kazi ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ni kutafuta suluhu nasio kua sehemu ya kulalamika, kwahiyo usemi wa Kampuni ya Hero Hunter kwamba ' Piga gia mpaka Barabara ishangae' ni ujumbe tosha kwa wahalifu na watashangaa.
| Meneja Mkuu wa Kampuni ya Karemjee Jivanjee (KJL) William Kadiva. |
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Karemjee Jivanjee (KJL) William Kadiva amesema kwamba Kampuni hiyo imetoa msaada wa pikipiki tano aina ya Hero Huter 125 cc zenye thamani ya shilingi milioni 15, zenye uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 60 hadi 70 kwa kutumia mafuta kidogo ambayo ni lita moja.
" Leo Hero inatoa Pikipiki tano aina ya Hunter ili kuliwezesha Jeshi la Polisi Kufanya Doria za kila siku za kiusalama,hizi Pikipiki zinatumia mafuta kidogo kwa mwendo mrefu,tunatarajia kukuza uhusiano Kati ya viongozi wa Usalama na Kampuni yetu ya Karemjee Jivanjee ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi" amesema Kavida.
| Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akipokea nyaraka za makabidhiano ya Pikipiki tano kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Karemjee Jivanjee (KJL) William Kadiva. |
No comments
Post a Comment