Zinazobamba

Jioni ya leo kipindi kipya chenye matarajio ya kutoa full package, Oscar asema kitakuwa kipindi namba moja Tanzania




Mtangazaji mpya wa kipindi cha jioni ya leo Dina Marious  akizungumza katika hafla iliyoandaliwa jana

MTANGAZAJI maarufu nchini Dina Marious na mchambuzi wa soka Oscar Oscar watakuwa ni watangazaji wa kipindi cha JIONI YA LEO ambacho awali kilikuwa kikijulikana kama UBAONI kitakachakuwa kikirushwa na EFM.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Vipindi wa EFM Dickson Ponera akizungumza katika hafla fupi ya kubainisha majukumu yao mapya iliyofanyika Makao Makuu ya EFM na TVE Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa awali Dina Marious alikuwa akitangaza kipindi cha Uhondo huku Oscar Oscar akiwa ni mchambuzi wa kipindi cha michezo cha Sports HQ.

Aidha Ponera alisema kipindi hicho kitakuwa kikirushwa kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku.

Alisema wataungana katika kipindi hicho na Roman Shirima, Mpoki na Veronica Frank ambao walikuwa wakitangaza kipindi cha UBAONI.
Kuuguza watoto wawili wenye Siko Seli kwa kipato cha Tsh. 3,000 …“naumia roho” - Hawa

Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema - Pwani

Uso wake umejaa tabasamu muda mwingi lakini kuna nyakati tabasamu hilo hutoweka kabisa, Arafa Kambi ana Siko Seli.

"Ninakuwa na maumivu makali ya miguu au mikono na meno, ni makali… mara kwa mara nalazwa {hospitalini}, naongezwa maji, nikipona narudi nyumbani,” anasimulia Arafa, Mkazi wa Mkuranga Mkoani Pwani.

Siko Seli ni ugonjwa wa damu ambao mtu huzaliwa nao kwa kurithi vinasaba vya ugonjwa huo kutoka kwa wazazi wake wote wawili {baba na mama}. 

“Kwa hiyo narudishwa nyumbani, yakirudia tena maumivu yale makali, narudishwa hospitali, naongezwa maji. 

Arafa anasema hayo ndiyo maisha yake na kwamba hajawahi kubahatika kabisa kwenda shule, hajui kusoma, kuandika wala kuhesabu. 

“Napenda niwe kama wenzangu, wanacheza vizuri… lakini mimi nikicheza nahisi maumivu, sijui kusoma wala kuandika, natamani pia nijue… wengine wananinyanyapaa,” anasema. 

Hawa ni mama yake na Arafa, katika mahojiano maalum na MATUKIO NA MAISHA BLOG hospitali ya Wilaya Mkuranga, anasimulia safari ya maisha ya mwanawe huyo tangu akiwa na umri wa miezi mitatu hadi sasa. 

“Akiwa na miezi mitatu, anaumwa mikono inalegea, anapiga kelele, nikawa nawagombeza wanangu wakubwa {zake} {“mmemdondosha, wananiambia… hapana”}. 

“Mara mkono unavimba, nilihangaika naye, kipindi hicho hapa hospitali {ya Wilaya Mkuranga} bado hili tatizo walikuwa hawawezi kulitambua. 

“Akiwa na miaka miwili kuna hospitali ilifunguliwa kule Kiparang’anda, nilikwenda daktari alimpima na kunipa jibu anaumwa Siko Seli. 

JE ALIFAHAMU NI NINI? 

Anaongeza “Nilijiuliza inakuwa-kuwaje, nakumbuka daktari aliniambia ni upungufu wa damu, alinipa maelekezo damu yake inavyokuwa, alinianzishia dozi, hata kama sina hela alinipa {dozi} yote. 

“Narudi nyumbani, nahangaika nikipata hela nalipa. Nimeenda hivyo hadi yule daktari akaenda kusoma, hapo ilibidi nichukue zile nakala nije huku Mkuranga {hospitali ya wilaya}. 

“Nilianza kuchukua dawa hapa, akaendelea vizuri, niliugua nikashindwa kumpeleka kliniki yake akakosa huduma, alikata dozi.

Anasema kwa kuwa alikosa dozi zake hali yake ilianza kutetereka na uchumi wa familia yake uliyumba kwani mumewe naye alianza kuugua na hadi sasa yu kitandani, maisha yao yamezidi kuwa magumu zaidi.

Arafa akizungumza na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

SIKO SELI ILIVYO

Ni ugonjwa wa damu ambao mtu huzaliwa nao pale anapokuwa amerithi vinasaba vya ugonjwa huo kutoka kwa wazazi wake wote wawili. 

Wanasayansi wanaeleza, kibaiolojia chembe hai nyekundu za damu huishi siku 90 hadi 100 kisha kuzeeka na kufa, lakini kwa mwili wa mtu mwenye Siko Seli chembe hizo huishi kwa muda wa siku 10 tu na kufa.

Hii inamaanisha kwamba mwili wa mtu mwenye ugonjwa wa Siko Seli huziharibu mapema chembe hai nyekundu za damu kuliko mtu asiyeugua ugonjwa huo.

Aidha, mwili wa mgonjwa wa siko seli huwa unatengeneza nyongo kwa wingi na hivyo kushindwa kukaa kwenye kifuko.

Hali hiyo husababisha nyongo kutoka nje ya kifuko chake na kusambaa sehemu mbalimbali za mwili na mgonjwa ndiyo maana mgonjwa huwa na rangi ya njano hasa machoni.

Wanaeleza bandama ya mgonjwa wa Siko Seli huongezeka ukubwa ili kufanya kazi ya ziada kuchoma chembe - chembe hizo.

Mgonjwa wa Siko Seli hupata maumivu makali ya mwili wakati mabadiliko hayo yanapotokea, athari kubwa zaidi anayoweza kuipata ni kupooza mwili hasa anapocheleweshwa kupelekwa hospitalini kupata matibabu sahihi.

Nchini Tanzania tafiti zinaonesha asilimia 15 ya Watanzania wana vinasaba vya ugonjwa huo, hata hivyo wengi bado hawajitambui.

Shirika la Afya Duniani {WHO} linakadiria kila mwaka Tanzania, watoto 8,000 hadi 11,000 huzaliwa na Siko Seli, hii ni sawa na watoto wanane katika kila watoto 1,000.

Barani Afrika nchi ambazo zimeathiriwa mno na ugonjwa wa siko seli ni Tanzania, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Kongo.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya Tanzania kuna zaidi ya wagonjwa 200,000 wa Siko Seli na ugonjwa huo huchangia asilimia 6.7 ya vifo vyote vya watoto chini ya umri wa miaka mitano, ikiwa ni sawa na watoto saba kati ya 100 wanaofariki kila mwaka.

Tafiti zinaonesha mikoa yenye idadi kubwa ya wagonjwa wa siko seli ni Kagera, Mara, Shinyanga, Kigoma na Geita ambayo ipo katika Kanda ya Ziwa.

Mikoa mingine ni Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara ambayo ipo katika Ukanda wa Pwani, lakini hiyo haimaanishi kwamba mikoa mingine hakuna ugonjwa, bali upo kwa kiwango cha chini.

HALI ILIVYO MKURANGA

Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, ilianzisha kliniki ya Siko Seli kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wagonjwa wenye Siko Seli Tanzania Julai, 2021, baada ya tathmini kuonesha Muhimbili ilikuwa ikipokea watoto wengi kutoka Mkuranga.

“Kliniki ilianza na watoto kati ya 75 hadi 100 na sasa kwa siku inaona watoto zaidi ya 20, kule Muhimbili ilionekana watoto wengi wanatokea Mkuranga na ilikuwa changamoto wengi hawarudi kliniki kwa sababu ya gharama,” anasema Daktari msimamizi wa Kliniki hiyo, .

Anaongeza “Ukanda huu {wa Pwani} Siko Seli huku ipo juu kwa sababu ya ‘inter marriage’ yaani unakuta mtu kaolewa, kaachwa anaolewa kwengine na hawana elimu ya afya ya uzazi, mtu hajui kwamba anapaswa kuchunguza afya yake kabla ya kuoa/kuolewa, wanaoana tu.

“Kwa hiyo unakuta wimbi kubwa la Siko Seli lipo huku, watu wanajua kupima Ukimwi tu hayo maradhi mengine hawajui, wanajua tu Siko Seli ni ugonjwa wa kuongezewa damu.

“Sasa hivi tunajitahidi kutoa elimu, mtu anapokuja na mgonjwa tunamuelimisha… wameanza kuelewa tunakaza mwengi tufike mahala jamii iwe na uelewa vizuri zaidi kila mtu awe na hiyo elimu,” anasema Dkt.  

KIPATO DUNI  

Hawa anasema alibeba ujauzito wa mwanawe mwingine na kujifungua kwa upasuaji, ambaye naye amegunduliwa ana Siko Seli.

“Alianza makelele {analia}, nikakuta ile hali ya kulegea, nikajua haya ndiyo kama yale {dalili alizoonesha Arafa}, nikarudi hospitali, alichunguzwa na kukutwa kesi ni ile ile {ana Siko Seli,” anasimulia Hawa. 

Anaongeza “Nilipohangaika naye huyu {mdogo}, kazi zangu zikavurugika, akaumwa mguu, nikaja naye kulazwa, nikakuta kavimba. 

“Tulienda hadi Muhimbili {Hospitali ya Taifa na kuruhusiwa}, lilitokea jipu likatumbuka, nikatafuta salio {nauli} nikaenda tena Muhimbili. 

“Tuliambiwa mguu wake mmoja umeathirika {umepata hali ya ulemavu}, tulifika hadi MOI {Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili} walipiga picha, nyingine walibaki nayo na nyingine ninayo nyumbani,” anasimulia.

Makuti aliyoyavuna kutoka kwenye minazi, kuyasuka kiustadi kisha kuyauza kwa watu ambao huyatumia kuezekea nyumba au sehemu zao za biashara, yaliweza kumuingizia kipato kati ya Tsh. 30,000 hadi 60,000. 

“Sasa hivi kila mtu anaezeka bati atakuona wewe {msuka makuti}, sasa sina uwezo kutwa niko njiani nauguza, utalima!!!? Kila kitu kwangu ni shida,” anasema. 

Anabainisha kwamba sasa ameamua kugeukia uchongaji wa chelewa {vijiti ambavyo hupatikana baada ya kuparura makuti ambavyo hutumika kutengeneza mafagio, hata hivyo kipato ni duni. 

“Nikichonga chelewa mkono mmoja nauza Tsh. 3,000, wakati zamani nilikuwa nasuka makuti matajiri wapo… mkono mmoja Tsh. 3,000 sasa hivi upate mikono mingapi upate Tsh. 60,000?!. 

“Makuti yanaingia kidogo, chelewa zile zinaingia nyingi {kwenye kiganja cha mkono}, upate Tsh. 60,000 ni kazi ndefu sana. 

Anasema kuendesha maisha yao pia ilimlazimu kulima hususan mihogo shambani kwake ili wapate chakula lakini sasa hawezi pia kulima kwani amezeeka.

Anaongeza “Sina kitu, imebidi nihangaike kila sehemu angalau nipate japo bima iwasaidia hawa vijana imeshindikana, nimeelemewa. 

“Dawa sina, naumia na roho kuwalea, uwezo sina kusema nitalima kibarua nipate hela, kuna muda silali najifikiria mimi nina nini!!?. 

“Huyu mdogo miguu haina nguvu, shule ni gharama hawezi kutembea kuna mwendo wa saa moja, inabidi apande bodaboda, nauli sina ni changamoto. 

Anasikitika “Dawa sina, naumia na roho kuwalea, uwezo sina kusema nitalima kibarua nipate hela, kuna muda silali najifikiria mimi nina nini!!!. 

Arafa akifurahia jambo wakati wa mahojiano na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

NISAIDIENI BIMA 

“Kwa hali niliyonayo na mwenzangu yupo kitandani anatumia dawa endelevu, ana cheti cha uzee lakini dawa ananunua vile vile. 

“Nikienda Muhimbili si chini ya Tsh. 60,000 hadi 70,000 makaratasi yapo kule nimeshindwa kununua, vipimo unalipia, dawa unanunua sina uwezo huo. 

Anaongeza “Kutoka nyumbani hadi stendi Tsh. 4,000 nikitoka hapa hadi Muhimbili hela nyingi hata Tsh. 50,000 au 60,000 kwangu ni ndogo. 

“Naiomba Serikali/wananchi wenzangu wanisaidie bima tu, mambo ya kula yote yapo pembeni najijua mwenyewe, wanangu wakila mimi hata nikinywa maji naridhika. 

“Kula najijua mimi… nisaidiwe tu bima ya kuuguza watoto basi,’ anatoa ombi lake. 

Msomaji wetu umeguswa na simulizi ya Hawa na familia yake, wasiliana nasi kwa simu nambari +255 758 218 013 tuweze kukuunganisha nao. Karibu.

Post a Comment

saba


 

nane


 


sita

Responsive Advertisement

No comments