Zinazobamba

DC Ludigija ataka Mkampuni ya Urasmishaji yahuishe Mikataba Yake Ndani ya Siku Saba.

 

Na Mussa Augustine.
MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzi  Ludigija ameyataka Makampuni yote yanayofanya kazi ya kurasimisha ardhi katika wilaya hiyo ambayo mikataba yao imeisha Muda wake kuihuisha mara moja ndani ya siku 7
Agizo hilo amelitoa Jana Dar es salaam katika kikao kazi na kamati ya Ardhi ya Wilaya iliyojumuisha wenyeviti wa Mitaa, Makampuni ya ardhi, ambapo kupitia kikao hicho imeonekana Makampuni yaliyo mengi yaliyoingia mkataba ya kufanya kazi ya kurasimisha ardhi mikataba imeisha Muda wake na kazi haijafanyika kwa asilimia kubwa 

"Karibu mikataba yote ambayo kamati hii iliingia na Makampuni mingi imeshakwisha muda wake na Kwa utaratibu kama kuna hela ya mtu umeichukua lakini mikataba imeisha hakuna namna ya kutaka kuihuisha na wananchi hawajui hatima yao lazima kamati iliangalie hili alisema Ludigija

Hata hivyo alisema amechoka wananchi wengi  wakilalamikia eneo hili la urasimishaji huku migogoro ya ardhi ndani ya Wilaya hii imekuwa mingi ikiwa mingi sababu  inayosababisha ni maeneo wanauoishi hajapimwa wala hawajapewa hati miliki na mikataba ya Makampuni iliyopewa kufanya kazi imeisha Muda wake na  wananchi wakiwa wamelipa fedha 

"Wapo watu ambao wamekuwa wakiishi kwa ujanja ujanja hapa mjini wamachinga mihuri ya watendaji na wenyeviti huwa wanatengeneza nyaraka na kumrudisha nyuma miaka na kukutana na viongozi ambao wameshato kwenye madaraka na mwisho wa siku mtu eneo ni la kwake ni halali analimiliki akienda kwenye mkono wa sheria kupitia nyaraka hizo za kutengenezwa anaambiwa eneo siyo lake"alisema Ludigija

Katika hatua nyingine amesisitiza wenyeviti wa serikali za Mitaa kuitisha mikutano kwenye maeneo yao yote wananchi waambiwe kufanya urasimishaji siyo suala la hiari ni la lazima kwani wanapopata migogoro huiangukia serikali kuitatua ili kero hiyo iishe ni kurasimisha maeneo wanayoyamiliki  na kupata hati miliki

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mkoa wa Dar es salaam Idrisa Kayela amesema changamoto katika suala hilo la ni wananchi kutokuwa na elimu na baadhi yao kukosa fedha ya kulipia fedha ya urasimishaji ili wapewe hati miliki.

"Wananchi wanasababisha suala hili kusuasua kwani wanapopimiwa eneo na kuwekewa bikoni wanabeza na hawalipii wanaridhika hivyo kuonekana waliopimiwa ni wengi lakini waliolipia ni wachache hata robo yake haifiki  hivyo wenyeviti waende kuwapatia wananchi wao elimu 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kata ya Mogo George Mtambali alisema katika eneo lake limepakana na Tazara baadhi ya wananchi wamevamia  maeneo hayo na kuyajenga ukiangalia wengine ni wastaafu hivyo serikali iliangalie suala hiilo kwa makini inwe namna ya kusaidia wananchi hayo 

Hata hivyo Mkurugenzi wa Kampuni Independent Planners Limited  ya Clemence Mero alisema serikali imekuwa nyuma kuhimiza wananchi wake kuchangia gharama za urasimishaji kufanya jambo hilo kuwa la lazima kwani watu wengi hawaioni kuwa siyo salama kukaa kwenye eneo ambalo halijarasimishwa hivyo inapelekea kampuni kufanya kazi kubwa na ngumu kwao 


No comments