COSTECH ,NORTHEASTERN UNIVERSITY wakutana Kujadiliana Athari za Mabadiliko ya Tabianchi
Na Mussa Augustine.
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia( COSTECH) imepata ugeni wa watu wapatao 35 kutoka chuo kikuu cha Northeastern University cha Buston Nchini Marekani ambao wamekuja kwa ajili ya warsha ya kujadiliana kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi,Ustahimilivu na Maendeleo endelevu.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam na waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa kutoka COSTECH Samson Mwela amesema kwamba warsha hiyo inalenga kujadiliana namna ya kushirikiana kwa pamoja kupitia program wanazojifunza chuoni ili kuweza kutatua changamoto inayoiathiri dunia kwa sasa ya Mabadiliko ya Tabianchi.
Aidha amesema kuwa kupitia majadiliano hayo wataimarisha mahusiano kati ya chuo kikuu cha Northeastern pamoja na vyuo vya hapa nchini kwa kushirikia na COSTECH ili kufanya tafiti za kisayansi ili kusaidia kutokomeza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Marekani wanateknolojia na maarifa hata sisi pia tunayo hivyo leo tunajifunza kutoka kwao na wao wanajifunza kutoka kwetu na tumewaalika chuo kikuu cha Maji, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) pamoja na Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu na kuja na makubaliano ya pamoja ya namna ya kutatua changamoto hizi za mabadiliko ya tabianchi” Amesema Mwela.
Ameongeza kuwa sayansi na teknolojia inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa Taifa hivyo COSTECH kama waratibu wakuu wa Sayansi teknolojia na ubunifu wanayowajibu wa kuwaunganisha watafiti wa ndani na nje ya nchi ili wafanye tafiti zenye tija kwa maslahi ya taifa.
![]() |
| Mhadhiri wa chuo kikuu kushiriki cha Sayansi na tiba Muhimbili (MUHAS) Dkt. Khadija Malima. |
Kwa upande wake Mhadhiri wa chuo kikuu kushiriki cha Sayansi na tiba Muhimbili (MUHAS) Dkt. Khadija Malima amesema kutokana na program ya pamoja ya wanafunzi wa miaka yote inayofanywa na chuo cha Northeastern ujio wao utasasidia kuleta hamasa kwa vyuo vya hapa nchini.
Amesema kwamba majadiliano hayo pia yatasaidia kutambua namna mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri afya ya Binadamu hususani katika janga linaloisumbua dunia kwa sasa la Uviko-19.
![]() |
| Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Ladislaus Chang’a. |
Naye Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Ladislaus Chang’a amesema ushirikiano huo utaenda kujibu namna tunavyoweza kushirikiana katika tafiti na kukabiliana na matatizo ya tabia ya nchi.


No comments
Post a Comment