Nass Sports Solution yazindua shindano la After School Clash
Na Mussa Augustine.
Kampuni ya Nass Sports Solution ambayo inainua Vipaji vya michezo kwa vijana imeanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na sita yanayoitwa After Shool Clash kwa lengo la kuwaunganisha vijana hao wakati wakisubiri kujiunga kidato cha tano na vyuo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayofanyika katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nassoro Mungaya amesema kwama hadi sasa timu 8 zimejisajiri kwa ajili ya mashindano hayo huku akiongeza kuwa zawadi mbalimbali zinatarajiwa kutolewa.
Aidha amesema kwamba mashindano hayo yatafanyika kwa makundi ambapo kuna kudi A na B yenye timu 4 kila kundi ,nakwamba mshindi wa kwanza anatarajiwa kupata kombe na medali,mshindi wa pili na watatu watapata Medali.
Vilevile amesema kutakuwepo na zawadi kwa mfungaji bora,mchezaji bora pamoja na golikipa bora ,hivyo ameomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kumuunga mkono kufadhili michezo hiyo kwani inalengo la kuibua vipaji kwa vijana.
"Tuna timu 8 zitakazochuana vikali katika mashindano haya ya After Shool Clash, tuna timu ya Alpha High School, Ahmes Secondary School,Crown Secondary School,Rosmin Secondary School,Marian Boys Secondary Scool,St.Joseph Boys Secondary School ,Heritage Secondary School,Abbey Boys Secondary School" amesema Mkurugenzi huyo.
No comments
Post a Comment