Zinazobamba

MAIMUNA SAIDI AREJESHA FOMU NDANI YA CHAMA CHAKE CHA "ADC" ASUBIRI KIBARI CHA CHAMA KWENDA KUWANIA USPIKA WA BUNGE.

 Na Mussa Augustine.

-
Kada wa Chama Cha Alliance For Democratic Change( ADC) Bi Maimuna Saidi amerejesha fomu aliochukua Januari 16 makao makuu ya Chama jijini Dar es salaam kwa ajili ya Kuomba Kuteuliwa na chama chake  kugombea Nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza mara baada yakukabidhi fomu hiyo kwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara wa ADC, Bi Maimuna amesema kwamba ameamua kugombea nafasi hiyo nakwamba endapo atateuliwa na Chama chake nakuweza kushinda nafasi ya Usipika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anaunganisha mihimili ya serikali ambayo ni Mahakama,Bunge na Serikali ili ifanye kazi kwa ushirikiano.



"Nina haki yakikatiba kugombea nafasi hii ya Uspika,pia nitahakikisha Bunge linakua na ushirikiano na mihimili mingine ili ifanye kazi kwa pamoja kwa kufuata haki sawa katika kusimamia ,kukosoa na kushauri serikali,amesema Bi Maimuna.

Nae Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara   Bw. Doni Mnyamani amesema kwamba hadi sasa bado kada mmoja wa chama hicho kajitokeza kuchukua fomu yakuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakwamba Kikao cha kamati tendaji ya Chama hicho inatarajiwa kuketi Januari 20 kwa ajili yakupitisha jina la mgombea mmoja ili lipelekwe Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

" Leo Bi Maimuna Saidi amerudisha fomu mbayo alichukua jumapili ya tarehe 16 kwa ajili ya Kuomba kugombea nafasi ya Usipika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya aliyekua Spika wa Bunge hilo Job Ndugai kujiuzulu, mpaka sasa tuna mtu mmoja tu aliejitokeza kuchukua fomu " amesema Bw.Mnyamani

Nakuongeza kuwa  "tarehe 20 kamati  tendaji ya ADC itakutana kupitisha jina la mgombea mmoja kati ya wale watakaojitokeza kuchukua fomu na jina hilo kulipeleka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya taratibu zingine,lakini tunaendelea kupokea wengine watakaopenda kuja kuchukua fomu.

No comments