ADC yampitisha rasmi Maimuna Saida Kassim kuwa Mgombea Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Na Mussa Augustine.
Chama Cha Alliance For Democratic Change kimempitisha rasmi Maimuna Said Kassim kuwa Mgombea wa Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku kikiwataka wabunge kumpa kura za ndio bila kujali itikadi za kisiasa.
Akizungumza Mwenyekiti Taifa wa ADC Hamad Rashid Mohamed amesema kwamba chama chao kimempitisha Maimuna baada ya kamati tendaji ya Chama hicho kujiridhisha kuwa anauwezo na elimu ya kutoshaz pia ana weledi mkubwa hivyo anaweza kuwaongoza wabunge kama kiongozi mkuu wa Mhimili huo.
Aidha amesema kwamba pamekuwepo na kasumba kwamba ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa wabunge wa chama tawala kumchagua Spika anaetokana na chama chao bila kujali uwezo wake ,hali ambayo inachangia kuleta migongano yakimihimili katika nchi.
" Hatuna mashaka hata kidogo na uwezo wa Maimuna Said kwani hata katika uchaguzi mkuu uliopita aligombea ubunge katika jimbo la kilindi na alipata kura elfu kumi na nane,hivyo ana uwezo wakusimamia nakuliongoza bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" amesema Mwenyekiti huyo.
Wakati huohuo Mwenyekiti huyo amesema Chama cha ADC hakipeleki mgombea kwa kutafuta CV kama inavyozungumzwa huko nje lakini Chama hicho kina amini katika misingi ya uongozi na hiyo ndio moja ya sifa ya chama na sivinginevyo.
Ameongeza kuwa chama hicho moja ya kazi yake ni kupika viongozi ambapo tayari wana kiongozi ndani ya serikali ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga na sasa wanakwenda kutoa kiongozi mwingine ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo amempongeza rais Samia kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya hasa kuwaunganisha watanzania na hata maendeleo yanaonekana katika kipindi hiki kifupi alichohudumu hivyo wao kama ADC wataendelea kumuunga mkono.
Kwa upande wake Mteule huyo ambaye ndo mgombea wa kiti cha Uspika Maimuna Said Kassim akizungumza mara baada yakutangazwa kuwa mgombea amesema kwamba anashukuru Chama chake kwa kumwamini ,nakumuona anafaa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
" Nilijitathimini nikaona nina uwezo,nina elimu ya kutosha na nimewahi kuwa kiongozi katika Chuo kikuu cha Dodoma,na nimesoma masuala ya kibunge hivyo nina hakika kama wabunge watanichagua nitafanya kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa" amesema Maimuna.
Nakuongeza kuwa "nataka kulifanya bunge kuwa la kisasa kwani katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na migongano ya kimihili ambayo inapelekea kila muhimili kusema la kwake hivyo endapo watampa ridhaa atahakikisha anakwenda kuunganisha na kufanya bunge kuwa imara zaidi. " amesisitiza
Maimuna ameongeza kuwa anaimani kubwa atakwenda kupata kura za ndio na watanzania wategemee mabadiliko makubwa yanakwenda kutokea katika kipindi changu cha uongozi.
No comments
Post a Comment