Wanazuoni waaswa kurithisha historia sahihi ya tanzania
Na Judith Mhina -Maelezo
Waziri wa Katiba na
Sheria Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Professa Palamagamba
Kabudi, amesema kazi kubwa ambayo wanazuoni wanayo ni kufanya utafiti na
kuhakikisha wanarithisha historia sahihi
lwa watanzania wa vizazi vya sasa na vijavyo.
Profesa labudi
ameyasema hayo wakati wa kufumgua kongamano
la maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika
lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA
kampasi ya Maruhubi.
Amesema kazi kubwa inahitajika katika kuhakikisha
utafiti wa kina unafanyila kuhusu Historia ya Tanzania, ma sio kujikita kwenye
historia ya siasa na uchumi tu na
kuacha eneo muhimu la hisrtoria
limalohitajika kuwarithisha vijana wa sasa na waabadaye.
“Wazee walio wengi
wanajua historia hiyo na kusimulia watoto na wajukuu zao, lakini hawa wazee
wakishaondoka kuna hatari ya historia hiyo kupotea kama haikufanyiwa kazi na
Wanazuani na kuiweka katika kumbukumbu zitakazo tumika sasa na kwa vizazi
vijavyo.” Amesisitiza Kabudi.
Uhuru wa Tanganyika
umeleta mshikamano ma ukomavu wa kudu,isha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao matokeo yake
yanaonekana katika kuleta maendleo kwa mwananchi mmoja mmoja, famikia na Taifa kwa ujumla.
Professa Kabudi, amesisiiza
kuwa unaposema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni lazima useme Uhuru wa
Tanganyika na Mapinduzi atukufu ya Zanzibar, ambao ndio msingi mkubwa wa
Muungano.
“Kongamano hili
kimejadili miaka 60 ya uhuru wa
Tangayika na tutakaposherekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miaka
michache ijayo tutakuwa tunajadili chimbuko, shina ambalo matokeo yake ni Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,”,Amesema,
Akelezea historia ya
uhuru wa Tanganyika uliofanyika tarehe 9 Desemba mwaka 1961 amesema ni siku
muhimu katika historia ya Tanzania kwani Tanganyika ilipata uhuru wake kutoka
utawala wa Muingereza ikiwa ni nchi ya udhamini ya Umoja wa Mataifa.
Amesema Watanganyika
na Wazanzibar walisherehekea siku hiyo ya Uhuru kwa matumaini ,makubwa ya
kujiletea maendeleo, kupata furaha, na
ustawi wa jamii husika kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimazingira ili kuwa na Taifa bora mambo
ambayo walikuwa hawayapati wakati wa kutawaliwa kutokana na mambo mawili makubwa ikiwemo ubeberu,ukoloni
na maamuzi ya watu waliohuru kuungana.
Alibainisha kwamba wajerumani
walipotawala haukuwa utawala rahimu kwani ndio uliozaa vita vya Majimaji mwaka
1905 mpaka 1907 ukiondoa vita vyengine vya kina Bushiri na wengine pamoja na
kushindwa katika vita hivyo lakini vilimfanya mkoloni kuona Watanganyika hawapo
tayari kutawaliwa.
Amesema sifa kubwa ya mapambano ya uhuru wa
Tanganyika Mwalimu Julias Nyerere alisistiza mambo mbalimbali kwa watanzania
ikiwemo kuishi pamoja bila ya kujali, dini, rangi wala kabila.
Akiongelea upande wa
Zanzibar pia vitimbi vya ubeberu na ukoloni havikwisha lakini kila njia
ilitumika kuhakikisha Zanzibar inabaki katika mikono yao na himaya yao.
Amesema jambo
linalowaunganisha watu wa Zanzibar na watu wa Tanganyika katika kupigania uhuru
ni kuanzishwa kwa Tanganyika Afrika
Association (TAA) Afrika Association Zanzibar na Shirazi Association.
Akiongelea jambo
ambalo halifahamiki na wengi ni mchango wa Zanzibar katika kupigania uhuru wa
Tanganyika Waziri huyo amesema ni mkubwa kwani watu wengi waliotoka Zanzibar
walikwenda kupigania uhuru wao kutokana na udugu walionao.
Kwa upande wa siasa
amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika jambo hilo kwani Chama cha
Mapinduzi (CCM) ni watu wa mashirikiano,
kuafikiana na pia wanaweka maslahi ya wananchi mbele kuliko jambo lolote.
Amesema Tanzania na Zanzibar
inapiga hatua kubwa za kimaendeleo hivyo aliwaomba wananchi kubadilika katika
kutangaza mafanikio ya nchi yao ikiwemo Zanzibar ambayo ina mafanikio mengi
yaliyopatikana.
Sambamba na hayo aliwasihi
vijana na wananchi kwa ujumla kuenzi tunu ya amani na utulivu wa nchi yao kwani
mambo hayo ndio itakayofanya serikali ya Umoja wa Kitaifa kufanya mambo makubwa
zaidi ya kimaendeleo ya leo na vizazi vinavtojuja.
“Kero za Muungano zipo zinatatuliwa na kufanyiwa kazi siku hadi siku
na kuzipa ufumbuzi kwa manufaa ya maslahi ya wote”. Amesema Kabudi,
Waziri huyo
akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya miaka 60 ya uhuru ya ‘Tanzania imara,
kazi iendelee’ alisema yapo mambo nane ambayo Tanzania imeyapata katika kipindi
hicho cha uhuru ikiwa ni pamoja na tanzania kuwa taifa na sio mkusanyiko wa
makabila yasio na umoja katika baadhi ya nchi nyengine zilizokuwepo Afrika.
Jambo jengine
alisema inasheherekea miaka 60 ikiwa na Muungano imara usiotetereka wa mataifa
mawili huru ambayo kwa hiari yaliamua kuungana, kuadhimisha miaka hiyo ikiwa
nchi imeingia uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa katika
Tanzania mkuza 2025 na kuwa nchi ya pili ya Afrika Mashatiki na kati wakati wa
kipindi kigumu cha ugonjwa wa Uviko 19.
Mafanikio mengine
alisema wanasherekea siku hiyo ikiwa
Tanzania imara na ikiwa taifa lenye kujiamini kuenzi tunu za Taifa ambazo ni umoja,
amani, mshikamano, utu, haki, heshima ya mwanaadamu, uhuru na demokrasia.
Waziri huyo amesema
Watanzania wanadhimisha uhuru wa nchi yao wakiwa taifa lenye uthubutu na moyo
wa kujitegemea na kujiamini kujenga nchi na kuboresha maisha na ustawi bila ya
kumtegemea mtu kwa kushirikiana na mataifa mengine yenye nia njema na maslahi
ya nchi.
Sambamba na hayo
alisema wanasherekea miaka hiyo wakiwa wameitangazia dunania kuwa utajiri na
maliasili zilizokuwepo nchini ni mali ya watanzania, kushihirisha kwamba
Kiswahili ambayo ndio lugha iliyotumika kupigania uhuru kuwa lugha ya ukombozi
na utambulisho wa hadhi na heshima ya muafrika aliyokuwepo katika bara la
Afrika na nje ya Afrika na kuwa lugha ya kimataifa.
Amesema imedhhiirisha
dunia ukomavu wa kisiasa na ukomavu wa katiba kwani ni mara ya kwanza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifariki akiwa madarakani lakini kutokana na
katiba iliyoimara madaraka yalihamia kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo
yalifanyika kwa amani na utulivu.
Aliwaisisitiza watanzania
wakati wanasherehekea miaka 60 ya uhuru kuendelea kuwaenzi viongozi wao
waliojenga taifa hilo akiwemo Mwalimu Julias Kamabarage Nyerere na Mzee Abeid
Amani Karume.
Amesema mpaka sasa
nchi ipo salama katika uongozi imara na madhubuti wa Rais Samia na Dk. Hussein
Ali Mwinyi katika kuhakikisha Tanzania
inasonga mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi
Dk. Khalid Salum Mohammed, alisema uhuru wa mwaka 1961 Disemba 9 na Mapinduzi
ya mwaka 1964 ndio yaliyozaa Muungano wao hivyo wanapaswa kuwakumbuka viongozi
wasisi wa uhuru, Mapinduzi na Muungano wa April 26 mwaka 1964 akiwemo Mwalimu
Julias Nyerere Hayati Abeid Karume na na wenzao ambao wamefanya kazi kubwa
mpaka leo taifa lipo mikono salama.
Alisema uhuru
umewapa watanzania heshima ya kujitawala wenyewe na pia umeleta heshima ya kutambulika
utu wa watu.
Dk. Khalid alisema Mapinduzi,
Muungano na Uhuru umedumishwa katika uongozi wote uliopita hivyo hawana budi
kuwapongeza hasa viongozi waliokuwepo hivi sasa madarani ikiwemo Rais
Samia kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuendeleza Uhuru, Mapinduzi na Muungano na
Rais Mwinyi kwa kuendeleza Mapinduzi na kuiweka nchi katika hali ya amani na
utulivu na kuleta maendeleo kwa kasi kubwa zaidi.
Sambamba na hayo
aliwataka watanzania kujitambua na kuheshimu historia ya nchi yao.
Mapema Makamu Mkuu
wa Chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA), Professa Mohammed Makame Haji, alisema
kongamano hilo lina lengo kusheherekea miaka 60 ya uhuru na kuakisi Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar na Mapinduzi ya mwaka 1964.
Alisema nchi mbili
hizo ziliungana sio tu kwa makaratasi bali zilikuwa na udugu wa kidamu hivyo
Uhuru na Mapinduzi ndio kielelezo cha udugu uliokuwepo kwa miaka mingi.
Alisema zanzibar
ikiwa ni sehemu ya tanzania na ndugu wa tanganyika wameamua kufanya komgamano
hilo ili kupata nafasi ya kuona yale mema waliyopata katika uhuru wa Tanganyika
na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika kongamano
hilo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo uhuru wa Tanganyik na maendeleo ya
kijamii, kisiasa na kiuchumi, miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, mafanikio na changamoto na mwelekeo wa SMZ na SMT
katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na Uhuru wa Tanganyika.
Maadhimisho hayo
ambayo yamezundiliwa rasmu Disemba 2 jijini Dodoma ambapo kauli mbiu yake
ni 'Tanzania imara, kazi iendelee'.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni