Sakata la eneno la MUM kuporwa… Scuba kutoa ufafanuzi?
Eneo lenye ukubwa wa
Zaidi ya hekari 300 lililo tolewa kwa ajili ya ujenzi wa tawi dogo la Chuo kikuu
cha waisalam cha Morogoro (Morogoro Muslim University–Dares salaam Campus) limeporwa
na mfanyabiashara SCABA SCUBA
Eneo hilo lililotolewa kwa chuo hicho na mfanyabiashara wengine kuunga mkono jitihada za waumini wadini hiyo kujikomboa kielimu bwana Mohamed Iqbal, linadaiwa kuporwa na SCABASCUBA katika mazingira ya kutatanisha Kwa mujibu wa barua ya malalimiko yanayotoka ofisi ya makamu mkuu wa chuo
Hicho Prof.Mussa J. Assad
ya tarehe 14 Julai mwaka huu 2021 kwenda kwa waziri mwenye dhamana ya utumishi na
utawala bora, Mohamed Mchengerwa iliyosainiwa yenye kumbukumbu namba MUM/ADM/DC/6/19
inaeleza kuwa tarehe 11 mach 2013 bwana Mohamed Ikbal Haji alikipatia chuo hicho
shamba la ekari 300 eneo la Lin-gato Kisarawe2 kwa ajili ya ujenzi wa kampasi ya
Dares salaam ya chuo kikuu cha Waislamu Morogoro ambapo inaelezwa kuwa bwana Iqbal
aliahidi kuongeza ekari nyingine 300 iwapo ujenzi utaanza. Shamba hilo lilikabidhiwa
kwa taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (Muslim Development Foundation MDF) ambao ndio
wamiliki wa chuo ‘’baada ya kupewa barua hiyo (barua ya umiliki wa eneo),uongoziwa
MDF ukijumuisha Makamu mwenyekiti wa Taasisi Mhe.Abdul Rahman Kinana, katibu mkuu
Balozi Dkt.Ramadhani Dau, na wajumbe wa bodi kwa nyakati tofauti walifanya ziara
kwenye eneo husika na katika kipindi chote hicho si chuo wala MDF walipata taarifa
kuwa ardhi hiyi ina mgogoro’’.Inasema sehemu ya barua ya Prof.Assad ‘’kwa sababu
ambazo hatuzijui, ardhi yetu iliporwa na Maafisa wa Ardhi wa Kigamboni wa
kishirikiana na bwana Scaba Scuba, uvamizi huo umepelekea kuu za baadhi maeneo hayo
kwa wananchi na kuondoa mabango pamoja na vigogo vya mipaka ya chuo iliyowekwa na
chuo kwa gharama kubwa’’.Alisema Prof.Assad katika barua hiyo Katika barua hiyo,
Prof Assad anasema kuwa mwaka 2014 Rais wa awamu ya nne mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete aliwahi kufanya ziara rasmi nchini Kuwait na aliwasilisha kwa mfalme wa
nchi hiyo maombi yanayoambata na na michoro
ya ujenzi wa kampasi hiyo kwenye eneo hilo la lingato ‘’tumefanya jitihada kadhaa za kulalamika kwenye
mamlaka husika ikiwemo TAKUKURU kwa kuandika barua kumbukumbu na MUM/ADM/D/7/110
ya tarehe26 Novemba 2018 lakini hadi niandikavyo barua hii hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa,
kinyume chake maafisa Ardhi pamoja na bwana SCABA wa naendelea kuuza maeneo hayo
kwa kasi kubwa sana’’.Iliongeza sehemu ya barua hiyo Taarifa za uhakika ambazo gazeti
hili linazo zinasema kuwa tarehe 11 machi 2013 mfanyabiashara Mohamed Iqbal alimwandikia
barua mwenyekiti wa MDF Marehemu Kitwana Kondo akimuarifu kuigawiaWAKFU taasisi
hiyo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro ‘’kwa hiyari yangu
nimeamua kuwapa Ardhi eneo la Kigamboni Mtaa wa Lingato Kisarawe, Eka 300 kwa ajili
ya ujenzi wa chuo kikuu cha waislamu. Iwapo mtaanza ujenzi mapema na nikiridhika
na matumizi ya ardhi hiyo basi nitawapa ekari nyingine 300’’ aliandika Iqbal ‘’Ardhi
hiyo nimeikabidhi mbele ya mwenyekiti wa MDF, Mheshimiwa Kitwana S.Kondo, MakamuMwenyekiti
wa MDF Mheshimiwa Abdulhamani Kinana, Katibu mkuu wa MDF Dkt.Ramadhani K. Dauna
Abbas M.Juma msimamizi wa eneo na mbele ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Lingato
bwana Cosmas Kalumanzila pamoja na viongozi wengine wa serikali za
mitaa……naomba nisisitize kuwa nimetoa Ardhi hiyo kuwa ni wakfu kwa ajili ya ujenzi
wa chuo au kwa matumizi ambayo yatasaidia kuendeleza chuo kikuu cha waislamu Morogoro
na Si vinginevyo’’.Inasomeka Barua ya Mohamed Iqbal kwenda kwa mzee kitwana kondo
Kitendo cha Profesa Assad ambaye alipata kuwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu
za serikali (CAG) kuwa kinatokana na unyeti wa wizara anayoisimamia waziri huyo
ambayo ni utawala bora na Prof.Assad anaonyesha kutokuridhishwa na watendaji wa
ardhi kigamboni katika kutekeleza utumishi uliotukuka ‘’Mheshimiwa Waziri, Tumeamua
kuleta malalamiko yetu kwako kwa sababu pamoja na kazi nyingine wewe ni waziri unayeshughulikia
utawala bora. Jambo ambalo ni dhahiri maafisa wa ardhi Kigambo ni wamekiuka misingi
yake’’.Amemalizia Prof.Assad
Hivi karibuni, waziri
Mchengerwa akizungumza na maafisa wa TAKUKURU katika mkutano wao wa mwaka huu 2021
alikaririwa
Akisema ‘’viongozi wengi
walio katika madaraka, katika nafasi mbalimbali hawatambui kwamba nchi hii ni ya
wananchi na wananchi ndio walio wachagua na wanapata mishahara na sifa na heshima
kwa sababu ya wananchi’’.Alisema MCHENGERWA aliongeza‘’ kati ya viongozi wengi wa
majiji makubwa wametekwa mifuko ni mwa matajiri, wadhurumaji na watoa rushwa, waonevu,
wanyonyaji, wasiolitakia memaTaifa lao, wameingia kwenye Pay Rol ya matajiri baadhi
ya viongozi, payroll ya matajiri wala rushwa, wanyonyaji wa haki za wanyonge kwa
fedha zao.. baadhi ya viongozi’’.Alisema Mchengerwa‘’Kamwe msikubali kuruhusu kudidimia
kwa matumaini ya mioyo ya watanzania kwa taifa lao. Mheshimiwa Rais anaamini kwa
umoja wenu na kwa ushirikiano na viongozi pamoja nawatumishi wengine wa TAKUKURU
mtaisaidia serikali anayo iongoza kujenga Tanzania ambayo wananchi wata nufaika
nayo na rasilimali watu, rasilimali za umma, kupata huduma bora pasipo kuombwa au kutoa Rushwa’’.Alinukuliwa Waziri Mchengerwa
alipokuwa akizungumza kwenye mkutano huo wa maafisa wa TAKUKURU wa mwaka huu 2021
Jitihada za kumtafuta mfanyabiashara SCABA SCUBA ilikupata ukweli wa uhusika wa
upande wake zinaendela
source Jamvi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni