TBL,GGM, NMB vinara ulipaji kodi
Serikali imewatambua na kuwapa tuzo walipakodi wakubwa ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.
Tuzo hizo zimetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi wakati wa Kongamano la
uwekezaji lililofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar
Katika tuzo hizo kampuni ya bia Tanzania Breweries Limited imeibuka
ya kwanza ikifuatiwa na kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu Geita Gold Mining na
nafasi ya tatu imeshikwa na Benki ya NMB.
Takwimu zinaonesha kuwa kampuni ya TBL imechangia kiasi cha
Shilingi bilioni 422 wakati kampuni uchimbaji wa Dhahabu ya Geita Gold Mining
imechangia kiasi cha Shilingi bilioni 338 na benki NMB ikiwa imechangia kiasi
cha Shilingi bilioni 252.
Kwa upande wa Zanzibar kampuni ya usafirishaji ya Azam marine
imeibuka ya kwanza kwa kulipa kodi ya Shilingi milioni 930 na nafasi ya pili
imeshikwa na Z hotel limited imelipa kodi ya jumla Shilingi milioni 436.
Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo
Kidata amewapongeza walipakodi waliopata tuzo na kutambuliwa na kuwa TRA
inathamini sana mchango wa makampuni na taasisi zote zinazolipakodi na tuzo
hizi ni kuchochea ulipaji kodi kwa hiari.
Kwa upande wake Kamishna wa walipakodi wakubwa kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) amesema serikali kupitia TRA imewatambua walipakodi hawa
wakubwa ili kutoa hamasa kwa walipakodi wengine waweze kulipa kodi kwa hiari na
kwa wakati ili serikali iweze kuwahudumia watanzania wote kwa kuwapatia huduma
bora.
"Huu ni utamaduni ambao tumekuwa nao kwa miaka mingi sasa,
lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokana na ulipaji kodi kwa hiari na kwa wakati,
nawahamasishe walipakodi wote kulipakodi ili watambulike na waone fahari ya
kuwa Mlipakodi mkubwa" amesema Kamishna Mregi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni