apigwa na radi hadi kufa akiwa anafanya mapenzi na mume wa mtu
Mkazi wa Kijiji cha Masweya Kata ya Mtunduru Wilaya ya Ikungi, Vaileth Hassan Mtipa (32) amefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa wanazini na mume wa mtu kwenye pagale la nyumba.
Tukio hilo ambalo linadaiwa kughubwikwa na usiri
tangu lilipotokea mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu lakini baadaye limeanza
kuzungumzwa huku ndugu wakikiri kutokea tukio hilo.
“Tukio lipo na tumeshamzika lakini uliza viongozi
watakuambia, na hadi sasa mwanaume aiyekuwa na marehemu bado anaugulia maumivu
kwani alijeruhiwa vibaya miguuni na radi hiyo,” alisema shuhuda wa tukio hilo.
Inadaiwa siku ya tukio hilo, Vaileth alikuwa na
mpenzi wake Hassan Nzige na wakati wanafikwa na majanga hayo kwenye pagale
walikuwa wakiendelea kufanya mapenzi.
Shuhuda anaeleza kuwa baada ya kupatwa na mkasa
huo, Nzige alishindwa kusimama ndipo akaanza kupiga yowe kwa nguvu kwa ajili ya
kuomba msaada ndipo watu wakamkuta akiwa hajiwezi wakati mwenzake akiwa
amepoteza maisha tayari.
Baadhi ya wanakijiji wa Masweya walimchukua Nzige
aliyejeruhiwa miguu yake na kumkimbizwa zahanati ya Ndulungu, kwa matibabu
ambapo inadaiwa kuwa kwa sasa anaendelea vizuri.
Mwenyekiti wa Kijiji Masweya, Saidi Hongoa amekiri
kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 23, 2021 jioni muda mfupi kabla mvua
haijaanza kunyesha.
“Radi ilipiga kabla mvua kuanza kunyesha, wakati
huo wapendanao hao wakiwa kazini (wakifanya mapenzi) na wote wawili
walikimbizwa katika zahanati ya kijiji cha Ndurungu wakati mwanamke akiwa
ameunguzwa vibaya shingoni na mgongoni na mwanaume alikuwa ameunguzwa miguuni,
lakini walipofikishwa waliambiwa mwanamke alikuwa amepoteza maisha tayari”,
amesema Hongoa.
Amesema baada ya kutokea kwa tukio hilo, juhudi
zilifanyika katika kumjulisha mume wake marehemu Violeth, Manase Nkungu
aliyekuwa mbali na eneo hilo lakini aliposikia alilipokea kwa masikitiko.
Diwani wa kata ya Ndurungu, Theresia Daudi amsema
kuna kila dalili kwamba marehemu Vailenth alifariki papohapo kwa vile
aliunguzwa sehemu nyeti za mwili wake japo ni vigumu kueleza.
Mume wa marehemu, Manase Nkungu akiwa na
masikitiko amesema hakutegemea kuwa angepata pigo kubwa la ghafla namna hiyo
katika kipindi ambacho alimwamini mkewe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni