Mhe. Gekul- Droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba Taifa CUP 2021 yatoka.
Shafi Dauda (kushoto) na Baraka Kizuguzo ambaye ni Afisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) wakichezesha droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano ya Taifa CUP 2021 |
Wadau
wa michezo wakishuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya
mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar
es Salaam. |
Na John Mapepele
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa
na Michezo. Mhe, Pauline Gekul leo, Disemba 7, 2021 ameshuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya
mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza katika tukio hilo amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kurejesha
mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesimama kwa miaka kadhaa.
Aidha amesema mashindano ya mwaka huu yameboreshwa tofauti na yale ya awali.
Amesema maboresho hayo ni pamoja na kuingiza michezo mitatu; soka
kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha kwa wanaume na wanawake ambapo
awali ulikuwa mchezo mmoja tu wa soka.
Pia amesema mashindano haya yameshirikisha pande zote mbili za
Tanzania ili kuwa na sura ya kitaifa
Ametoa rai kwa vyama vya michezo na mashirikisho kuja kwenye mashindano
hayo ili kuona vipaji vya wachezaji ambao wanaweza kuwachukua kwenye vilabu
vyao.
Akizungumzia dhana ya Taifa CUP amesema lengo la mashindano hayo ni kuwashirikisha wanamichezo kutoka mikoa yote nchini ambapo amesisitiza kuwa mashindano hayo yanasaidia kuleta umoja na mshikamano, kutoa ajira na
kuimarisha afya za wachezaji hao.
Akimkaribisha Mhe. Gekul
kutoa hotuba fupi kabla ya kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa Michezo
nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandlizi ya Taifa CUP, Yusufu
Omary Singo amesema droo hiyo
imechezeshwa kwa uwazi ili kuyafanya yawe
wazi zaidi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni