SODO NA IMANI ZA KISHIRIKINA
ADELADIUS
MAKWEGA -UWJ-B. MKAPA.
Hali
ya shule nyingi za msingi katika maeneo ya mijini nchini Tanzania kutokana na
uhaba wa maeneo katika maeneo zilipo shule hizo kumekuwa na shule mbili hadi
tatu. Katika maeneo hayo na maeneo mengine zimejengwa hadi shule ya sekondari.
Hilo
linafanyika kutokana na mitaa mingine kukosa maeneo ya kutosha. Kwa bahati
katika maeneo mengine yaliyobahatika kuwa na ardhi ya maeneo ya wazi kama
kulikuwa na viwanja kadhaa vya michezo maeneo hayo yamejengwa shule ili kuokoa
jahazi la kukosa maeneo ya shule.
Ni
jambo la kawaida kwa shule ya mijini yenye majina ya mtaa A na shule hiyo
kujengwa katika mtaa (B) mwingine. Jambo hilo linafanya wanafunzi hao pia
kwenda mwendo kidogo ili waweze kufika shuleni. Natolea Mfano kwa wakaazi wa
Mbagala Sabasaba, Temeke Dar es Salaam tangu awali wanafunzi wa shule za msingi
wamekuwa wakienda kusoma mwendo mrefu kidogo hasa Mbagala-Kizuiani, Mtoni
Kijichi, Mbagala Kuu, Nzasa na Kongowe. Mathalani ukifika shule ya Msingi
Mbagala Kizuiani pale hivi sasa pana shule mbili za msingi hata ukitembelea
eneo lenye shule ya Msingi Mtoni Kijichi lina shule mbili za msingi.
Shida
ni idadi kubwa ya wanafunzi katika maeneo yanayozunguka maeneo hayo. Hilo ni
jambo zuri na halina shida yoyote. Kiushauri serikali ilipaswa kununua eneo
jipya ambalo lipo jirani na mtaa ambao shule inapaswa kujengwa, mathalani mtaa
wa Kizinga, hapo serikali inanunua nyumba 15 alafu eneo hilo linajengwa shule.
Desturi
ya Tanzania ni kuwa maeneo mengi ya shule ukiyafuatilia wananchi wenyewe
walijitolea maeneo hayo bure ili kuruhusu kujengwa kwa taasisi za umma zikiwamo
shule.
Kiserikali,
ununuzi wa maeneo kwa kuwalipa kidogo wananchi ili kujenga shule ni hoja nzito
maana mwenye ardhi ni rais anaweza akachukua tu. Kwa hiyo wananchi wanajitolea
ardhi zao mara nyingi bure.
Ili
paweze kujengwa shule mpya na iwe jirani na wenye mahitaji ya shule hiyo
serikali inawajibu wa kununua nyumba za watu kadha ndipo kujenga shule ya
msingi /sekondari na hata zahanati. Sitaki kulizungumza sana jambo hilo juu ya
mipango miji na yule aliyekosea katika hilo kwani leo si mada yangu.
Shule
hizi moja mpya na moja ya zamani, zimetatua kero ya uhaba wa madarasa ya
kutosha kwa wanafunzi wa mitaa miwili lakini hazijatatua hoja ya umbali wa
kutoka nyumbani kwenda shuleni. Kwani alivyotembea, Baba yangu, nilitembea mimi
mwenyewe na ule umbali anaotembea mwanangu leo hii na kesho mjukuu wangu
atatembea hivyo hivyo.
Wanafunzi
wanaosoma katika shule hizo wanaotoka mtaa mmoja huwa wanatambuana kwa majina,
ukoo, kabila, dini na hata mahusiano baina ya familia na familia(mazuri/
mabaya.)
Asubuhi
wakati wakiamka wanajianda kuelekea shuleni kwa makundi ya ujirani huo.
Utasikia Deme…twende, Ashura twende shuleni. Hawa wanafunzi wanajuana hata kwa
uwezo wao wa kupambana na shida mbalimbali wakiwa njiani kuelekea shuleni.
Mathani
mwanafunzi anatoka Mbagala Bagdadi (Bughudadi) anasoma Mbagala Kizuiani ni
mwendo wa dakika kama 20 kwa mguu kwa kuwa hapo hakuna miundo mbinu ya usafiri wa
daladala. Bodaboda zinaweza kupita lakini ni gharama kubwa. Mwanafunzi anayesoma
Mtoni Kijichi na anakaa Mbagala Mbuyuni ni mwendo wa dakika 40 kwa njia za
mkato.
Wakiwa
njiani wanakutana na wanafunzi wenzao wakorofi, hata hawa wanafunzi wenyewe. Wakiwa
katika kikundi hilo linawafanya kufika salama shuleni na kurudi salama
nyumbani.
Katika
shule ya msingi Mtoni Kijichi kulikuwa na wanafunzi sita wanaotoka Mbagala 77
na Mbagala Misheni (Msalabani). Katika kundi hilo wanne walikuwa wa darasa la
kwanza, mmoja wa la saba na mmoja wa darasa la tatu. Hawa wa darasa la kwanza
walichokifanya kwa kuwa walikuwa wanatoka shuleni saa 5 asubuhi wanamsubiri
kaka yao wa lasaba hadi saa nane ili waweze kufika kwao salama, hili lilikuwa
kundi la wavulana.
Hata
katika makundi ya wasichana hali inakuwa hivyo hivyo wanakuwa na dada mkubwa wa
madarasa ya juu kwa dharura zozote zile wakiwa njiani na wakiwa shuleni. Hapa
katika kundi la wasichana ndipo suala la dharura ya ukuaji wa mabinti nayo linaonekana.
Inawezekana
kundi la wavulana likawasumbua wasichana lakini huyu msichana ambaye anaongoza
kundi la mabinti wanzake kurudi nyumbani mara nyingi lazima anakuwa na nguvu kiakili
na nguvu kimwili ya kujilinda na kuwalinda wasichana wenzake waende shule
salama na warudi nyumbani salama.
Mvulana
mwanafunzi anaweza akafawafanyia fujo mabinti, kesi hiyo itafika shuleni na
nyumbani adhabu itatolewa kote kote. Mvulani huyo lazima ataogopa kufanya fujo tena
inawezekana kei hiyo ikafika hadi kwa mwalimu wa madrasa/mwalimu wa dini
shuleni na kanisani. Tatizo ni fujo hiyo inapofanywa na raia tena kwa siri.
Hapa
kama nilivyozungumza kutokana na mahusiano mbambali ya jamii kamati za shule na
urafiki wazazi wa kike huwa wanaambiana, Bibie wanangu wanasoma hapo shuleni
nisadie, wakipata shida okoa jahazi.
Mkuu
msafara wa kike anaambia kuwa mwenzako akipata shida mpeleke kwa mama fulani
atamsaidia kulinga na taratibu za kabila hilo. Inawezakana kwenye kamati ndogo
za shule yaani ile ya afya na chakula na ile ya ushauri na unasihi wakiwa na mwalimu
mmoja wa kike anakuwa mwokoa jahazi .
Wapo
wanaokimbilia kwa walimu hawa, lakini wapo ambao wanaamini kuwa jambo hlo lazima
kushirikisha shangazi. kwa hilo. Wakati mwingine nilisimuliwa kuwa
mama/shangazi anaweza kufungua biashara jirani na shule katika kipindi kile
anachohisi kuwa mtoto wake amekaribia hatua hiyo. Likishatokea mama/shangazi
huyo anafunga biashara anaendelea maisha yake ya kawaida.
Jambo
hilo linatokana na imani moja kubwa kuwa baadhi ya jamii inatakiwa binti akipata
dharura hiyo mara ya kwanza anatakiwa kufanyia na nduguye tu kama nilivyosema
na kama akifanyiwa na mtu baki basi binti huyo inawezekana akapata shida, hiyo
ndiyo Imani yao iwe kweli au la..
Wengine
wakiamini kuwa kama binti akitumia sodo na adui akachukua sodo hiyo au kuiona
tu itatumika kufunga kizazi milele hatopata watoto.
Sasa
kama nilivyosema yote hapo juu namna jamii masikini inavyohangaikia suala hili
la jamii yake ili kusaidia kizazi kiweze kuwepo kutoka kizazi kimoja kwenda
kingine.Ni wajibu wa sasa wa serikali kulifanyia kazi suala hili la kupatikana
kwa sodo mashuleni mwetu.
Kulisistiza
hilo ukichukua mfano ulio hai kabisa ya Tanganyika kabla ya uhuru ilikuwa na
machifu wengi sana na kwa sasa ukitembelea maeneo hayo ni maeneo machache sana
utakutana na majengo yanayotambulisha machifu hayo lakini ukiingia katika jamii
hizo utakutana na mambo kadhaa ya jamii mazito kama haya niliyoyaandika ambayo
yanaishi tangu kizazi na kizazi.
Mambo
haya yanasaidia katika ustawi wa jamii na ustawi wa maisha ya binadamu. Jengo
litabaki limesimama lakini mtoto(kizazi) akiwepo atasimulia na kuendeleza pale
tulipoishia. Kwa kuwa bado nipo Benjamini Mkapa ngoja niendelee na kazi iliyonileta
hapa, nakutakia siku njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Hakuna maoni
Chapisha Maoni