Waombaji filamu kupata vibali ndani ya siku tatu, walio ndani masaa matatu= Bashungwa
Na Suleiman Magali
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Innocent Bashungwa amesema Uzinduzi wa
mifumo ya kidigitali wa BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA itasaidia sana upatikanaji wa huduma kama vile
vibali vya Uhakiki wa filamu, Leseni za uendeshaji wa Kazi za Filamu, Vitambulisho
na Vibali vya kurekodi filamu kwa haraka kwa wadau wa filamu sehemu yoyote
yenye mtandao wa intanet hivyo kupunguza kero na usumbufu kwa wadau hao
kusafiri hadi Dar es Salaam kufuata huduma hizo.
Kauli hiyo ya Mheshimiwa Bashungwa
imetolewa Novemba 22, 2021 katika hafla ya
uzinduzi
wa mifumo hiyo, Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa na Uzinduzi wa Samia Taifa CUP uliwahusisha wadau
utamaduni, sanaa na michezo mkoani Dar es Salaam.
“Waombaji wa vibali vya kuandaa filamu iliwachukua siku
thelathini kupata kibali; lakini kupitia mfumo huu waombaji wa vibali vya nje
watapata vibali ndani ya siku mbili na wale wa ndani watapata vibali ndani ya
saa tatu (3), Kupitia mfumo huu, wadau wanaoomba kuhakiki kazi zao watapata
huduma hii ndani ya siku mbili (3) lakini iliwachukua hadi siku thelathini
kupata huduma hii.” Mheshimiwa Bashungwa alikumbusha.
Aliongeza kuwa Mfumo utatoa fursa ya kupata vibali kwa wasanii
wanaofanya shughuli za sanaa nje ya nchi na kutowalazimu kurudi nchini pale
inapobidi kuongeza muda wa vibali vyao au pale wanapokuwa wamepata fursa
nyingine wakiwa hukohuko nje ya Nchi.
“Mfumo huu utasaidia upatikanaji na
utunzaji wa takwimu za sekta ya filamu ambapo takwimu hizi zitasaidia katika
kupanga mipango ya kuendeleza sekta kwa upande wa nyanja mbalimbali kama vile;
mafunzo na uwezeshwaji”
Pia mfumo huu utapunguza gharama za uendeshaji kwa serikali
zikiwemo gharama za uchapaji vyeti vya usajili na vibali vya uendeshaji wa
shughuli za filamu na Michezo ya Kuigiza kwani vibali husika vitapatikani
kupitia mfumo.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni,
Vijana na Michezo wa Zanzibar Bi Tabia Mwita amesema kuwa anapongeza ushirikiano
uliopo baina ya serikali hizi mbili.“Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiana katika
mambo haya kama la usajili kwa kutumia mfumo wa kidigitali na kuanza rasmi kwa Samia
Taifa CUP kuwa yanaonesha umoja wetu kwa vitendo.”
Awali akitoa neno la kumkaribisha Waziri Bashungwa, Katibu
Mkuu wa WUSM Dkt Hassan Abbasi alisema kuwa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa
itawapa nafasi wasanii kupeleka maombi yao huko na yatapatiwa majibu.
“Uzinduzi wa Bodi hii leo unatoa nafasi ya mfuko huu kufanya
kazi yake vizuri na upya ambao kwa hakika utawezesha wadau kupata mikopo na
mafunzo na kusahau yaliyopita.”
Katika Hafla hiyo ilibainika kuwa Taifa Cup hapo awali ilikuwa
inashirikisha mchezo wa soka tu na hata timu ya taifa ilikuwa na wachezaji
kutoka kila mkoa na sasa Taifa CUP
itajumuisha kwa michezo zaidi ya mmoja yaani soka, mpira wa pete na riadha.
Mashindano haya yatakusanya washiriki wa bara na Visiwani, kuanzia tarehe 10
hadi 21 Disemba 2021. Huku nafasi ya
kuongezeka kwa michezo zaidi ipo wazi na kamati kushauri juu ya michezo mipya
zaidi.
Shughuli hii ni kwanza kufanyika tangu WUSM kuundwa rasmi
ambapo imewakutanisha wadau zaidi ya mia mbili na ushehee wa sekta za utamaduni,
sanaa na michezo.Huku Naibu Waziri wa WUSM Bi Pauline Gekul, Naibu Katibu Mkuu
Dkt Ali Possi, Wakurugenizi, wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara hii,
machifu na wadau kadhaa wakishiriki pia.
Nukuu
“Waombaji wa vibali vya kuandaa filamu iliwachukua siku
thelathini kupata kibali; lakini kupitia mfumo wa kidigitari waombaji wa vibali
vya nje watapata vibali ndani ya siku mbili na wale wa ndani watapata vibali
ndani ya saa tatu (3), Kupitia mfumo huu, wadau wanaoomba kuhakiki kazi zao
watapata huduma ndani ya siku mbili, huko nyuma iliwachukua hadi siku
thelathini kupata huduma.” Mheshimiwa Bashungwa alikumbusha.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni