Askofu Amon Kinyunyu: Chagua mwenyewe kuwa ng'ombe au Nguruwe
Jumapili ya Novemba 21, 2021 waumini mjini Dododoma walishiiriki
ibada ya uzinduzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya
Dodoma Usharika wa Chamwino Ikulu Mtaa wa Nazareth Buigiri. Ibada hiyo ya
uzinduzi wa kanisa iliongozwa na Baba Askofu Amon Kinyunyu ambaye ndiye Mkuu wa
Kanisa hilo kwa Dayosisi ya Dodoma.
Baba Askofu Kinyunyu wakati wa utangulizi wa mahubiri yake katika
ibada hiyo alitolea mtano suala la mtu anayekula nyama ya Ng’ombe na yule alaye
nyama ya Nguruwe. Kulingana na imani ya Kikristu zote hizo ni nyama halali, Je
Baba Askofu Kinyunyu alisema nini?
Baba Askofu Kinyunyu akitolea mfano huu kwa mtu anayekula nyama ya
ng’ombe kwanza kabisa mtu husika uandaa mnyama huyu na kumchinja, akishachinjwa
mnyama huyo ngozi ya ng’ombe inatenganishwa na mnyama alafu nyama yake hukatwa
vipande vipande kuchukuliwa na mpishi kwa ajili ya kupikwa na kuliwa.
Mara baada ya nyama kutenganishwa, ngozi ya ng’ombe huanikwa
vizuri sana kwa ajili ya matumizi mengine iwe kama kuwambia ngoma, kutengenezea
viatu, mikoba na mikanda na kadhalika.
Kwa yule anayetaka kula nyama ya nguruwe anapaswa kumchukua mnyama
huyo na kumchinja alafu kuikatakata nyama hiyo katika vipande na yule mpikaji huichukua
na kuipika na kuwa tayari kuliwa.
Baba Askofu Kinyunyu anasema kuwa ngozi ya nguruwe huwa inaliwa
pamoja na nyama. Kwa hiyo nyumba aliyochijwa nguruwe ni vigumu kukuta ushahidi
wowote ule lakini nyumba iliyochinjwa ng’ombe ndugu yangu ushahidi unapatikana
Unaweza Kusema, “ Jamani mbona naona ngozi na mie naombeni kipande
cha nyama.”
Baba Askofu Kinyunyu alifananisha wanyama hao wawili na maisha ya
binadamu yalivyo, kila mmoja popote alipo iwe shambani, kwenye uvuvi kwenye
ufugaji au katika nafasi ya uongozi unaweza kuchagua kuwa kama mnyama gani kati
ya hao wawili.
Uamuzi wakuchagua kuwa ng’ombe au nguruwe upo katika matendo ya
yule anayetenda maana baada ya hapo ushahidi utaonekana iwe kuacha ngozi au
kutoacha kitu.
Baba Askofu Kinyunye alitolea mfano huo akiwapongeza wanausharika
wa Chamwino Ikulu, Mtaa wa Nazareth Buigiri kwa wale waliofanikisha ujenzi wa
Kanisa la Usharika huo ambapo alisema kuwa hata kama hawatakuwepo duniani
ujenzi wa jengo hilo utakuwa sawa na yule aliyechinja ng’ombe na kuila nyama
yote lakini ngozi imesalia na kila mmoja wetu anaiona.
Kwa hiyo kila mmoja anayo nafasi ya kuchagua mnyama wake iwe
nguruwe au ng’ombe, Je wewe ni nani? Msomaji wa Makala haya nakupa muda wa kutafakari
hapo ulipo au popote ulipo angalia jamii yako alafu mchagulie anayekuongoza
kati ya wanyama hao wawili.
Waumini walijenga Kanisa hilo lenye
thamani ya shilingi za Kitanzania Milioni 300 kwa muda wa miaka 10 toka Disemba
4, 2011 hadi Novemba 21, 2021 ulipofanyika uzinduzi.
ambapo Baba Askofu Amoni Kinyunyu aliongoza
Ibada ya ufunguzi wa Kanisa hilo la kisasa likijengwa kwa michango ya washirika
mbalimbali wanaosali kanisani hapo ambapo ujenzi ulianza Disemba 4, 2011.
Awali akisoma
risala kwa baba askofu namna walivyojenga jengo hilo Mwinjilist Shekivuli
alisema, kanisa limejengwa kwa michango ya washirika hasa akimtaja Agrey Mwanri
ambaye alikuwa Naibu waziri wa Tamisemi katika kipindi hicho.
Ibada hiyo ilihusisha
kwaya tano ikiwamo Kwaya Kuu–Kutoka Kanisa Kuu, Kwaya Kutoka Chinangali, Kwaya
Kutoka Mkuhungu, Kwaya kutoka Kanisa la Anglikani Chamwino Ikulu tangu ibada ya
ufunguzi hadi ibada ya siku ya Bwana ambazo zote ziliongozwa na Askofu
Kinyunyu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni