Zinazobamba

TARURA wawanoa waandishi wa habari

Mkuu wa wilaya ya ilala Mh. Ng'wilabuzu Ludigija akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya waandishi wa habari na wahariri mapema jana jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Ng'wilabuzu Ludigija amefungua mafunzo yaliyoandaliwa na wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ajili ya kuwajengea uwezo Wahariri na  Waandishi wa  Vyombo vya Habari  pamoja na wadau wa sekta hiyo kuhusu Mfumo wa malipo ya Maegesho kwa njia ya Kielektroniki (TeRMIS) mapema jana jijini Dar es salaam.

Akiongea na wadau hao amesema kuwa mfumo huo unaotarajiwa kuanza kutumika tarehe 1 Desemba, 2021 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Singida na Mwanza na.

Ameongeza kuwa mfumo huo utasaisaidia serikali kukusanya mapato ambayo mwanzo yalikuwa yakipotea bure kwani mfumo ule wa mwanzo mwenye chombo aliwekewa risiti kwenye chombo chake mvua ikinyesha karatasi ikilowana basi pesa inapotea bure kwa kukosa ushahidi.

Ameendelea kwa kusema kuwa kila kitu kinachangamoto yake kwahiyo wananchi wavumilie tu baadae mambo yatakapokaa vizuri basi wataweza kuiona faida yake.
kwa upande wake Meneja wa Tarura mkoa wa Dar es salaam amesema kuwa Mtumiaji wa Maegesho anapaswa kulipia Ushuru wa Maegesho Kidigitali baada ya kupatiwa namba ya malipo (control number) ambapo atatumia Kumbukumbu namba hiyo kulipia maegesho kwa kutumia mtandao wowote wa simu ya mkononi, Benki ya NMB na CRDB au kupitia kwa Mawakala wa Huduma za fedha.

Mfumo huu wa Kidigitali unampa muda mtumiaji wa maegesho kulipia Ushuru wa Maegesho ndani ya Siku 14 tangu alipotumia Maegesho na endapo atashindwa kulipa ndani ya muda huo atatakiwa kulipa Ushuru wa Maegesho pamoja na faini ya Shilingi 10,000/=.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 500 kwa Saa na Shilingi 2,500 kwa Siku.

Mkoa wa Mwanza mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 500 kwa Saa na Shilingi 1,500 kwa Siku.

Mkoa wa Iringa mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa Siku.

Mkoa wa Dodoma mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa Siku.

Mkoa wa Singida mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa Siku.
Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari ikiendelea.
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Tarura mkoa wa Dar es salaam pamoja na mkuu wa Wilaya ya Ilala.

Hakuna maoni