Vikundi 100 vyapewa mmkopo wa Milion 918 Mlimba
Na mwandishi wetu
MBUNGE wa Jimbo la
Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amekabidhi hundi yenye thamani ya Sh
Milioni 918 kwa vikundi 100 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu pamoja
na kukabidhi Pikipiki 20 zenye thamani ya Sh Milioni 50 kwa vikundi viwili vya
vijana ikiwa ni sehemu ya mkopo uliotolewa kwa vikundi.
Akizungumza wakati
wa kukabidhi hundi hiyo na pikipiki hizo, Mbunge Kunambi amewataka Wanawake,
Vijana na wenye Ulemavu kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo isiyo na riba
inayotokana na asilimia 10 ya makusanyo ya ndani ya Halmashauri.
Kunambi amesema
kupitia mikopo hiyo wananchi wengi wataweza kuimarisha vipato vyao na kuchochea
maendeleo jambo ambalo limepelekea Halmashauri hiyo ya Mlimba kuongoza kwa
makusanyo ya mapato kwenye robo ya kwanza katika Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mara
ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo sambamba na kushika nafasi ya
saba Kitaifa.
" Niipongeze
sana Halmashauri yetu inayoongozwa na Mkurugenzi wetu Mhandisi Kaliwa ambapo
kwa pamoja akishirikiana na sisi Madiwani tumeweza kutenga Sh Milioni 275 na
kukusanya Sh Milioni 643 ikiwa ni fedha za marejesho ya mkopo wa miaka ya nyuma
na jumla yake ndio unapata Sh Milioni 918 ambazo leo tunazikabidhi kwa wananchi
wa Mlimba.
Niwapongeze wananchi
wangu wa Mlimba kwa kuwa waaminifu na kurudisha kwa wakati mnapochukua mikopo
hii kwani inasaidia kuwezesha vikundi vingine navyo kupata, kupitia mikopo
tunaenda kufungua uchumi wa Mlimba na kuimarisha maisha ya wananchi wetu, kwetu
ni Historia kubwa kukabidhi hundi yenye thamani hii katika Halmashauri yetu,
haijawahi kutokea," Amesema Mbunge Kunambi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba, Mhandisi Stephano Kaliwa amesema kuwa
Halmashauri hiyo imekua ikitenga kila mwaka asilimia hiyo na kuipeleka kwa
walengwa kama mkopo ili kuinua hali zao za kiuchumi na kijamii.
" Pamoja na
upelekaji wa mikopo hii Halmashauri itahakikisha kuwa fedha hizo zinarejeshwa
kwa wakati kulingana na makubaliano ya mkataba," Amesema Mhandisi Kaliwa.
Mkopo huo wa Sh
Milioni 918 umetolewa kwa vikundi 69 vya Wanawake vyenye mkopo wa Sh Milioni
570.5, vikundi 29 vya vijana vyenye mkopo wa Sh Milioni 339.5na vikundi viwili
vya walemavu vyenye mkopo wa Sh Milioni Nane.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni