MHE BASHUNGWA KUZINDUA MAMBO SITA YA KIMAGEUZI NA KIMKAKATI LEO
Na. John Mapepele, WUSM
Waziri wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa, (Mb), kesho, Novemba 22, 2021 atazindua
mambo sita ya kimageuzi katika Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mambo hayo
ni Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mfumo wa Kidigitali wa Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu nchini, COSOTA, Mashindano ya Michezo
ya Samia Taifa cup na kuwaunganisha wadau wa sekta hizo jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo. Dkt, Hassan Abbasi matukio hayo sita ya kimkakati na kimapinduzi yanakwenda
kutokea kesho wakati nchi yetu inaadhimisha mwaka miaka sitini ya uhuru wake.
Matukio haya ya kimkakati yatasaidia kuongeza ajira na
kuinua vipato na vipaji vya wasanii na wachezaji hivyo amewataka wasanii na
wachezaji kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia taaluma zao ili kuiingiza Tanzania kwenye ngazi za
kimataifa na kuinua uchumi wa nchi yetu.
“Kufufuliwa kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa na uzinduzi wa
Bodi utakaofanywa kesho utawawezesha
wasanii kupata mikopo ya masharti nafuu hivyo kupata wazalishaji,
watengenezaji, na wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo katika tasnia hii hapa
nchini” amefafanua Dkt. Abbasi
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa nchini. Dkt.Emmanuel
Ishengoma amesema kwa upande wa mifumo, kila mfumo wa
kidigitali katika kila taasisi (BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA) utasaidia wasanii
na waombaji wengine wa huduma
kwenye taasisi hizo ikiwemo
vibali vya matamasha na vibali
vya safari za nje kutoka popote walipo duniani
kupata bila kwenda katika ofisi za taasisi hizo kama ilivyokuwa
hapo awali, hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma, kupunguza muda na gharama.
Aidha, mfumo wa Kidigitali wa BASATA utasaidia kusajili wasanii
na kutoa vibali vya kuendesha shughuli za Sanaa ambapo Mfumo wa Bodi ya Filamu utafanya
kazi ya kusajili, kuhakiki filamu na
kutoa vibali vya kuendesha shughuli za filamu, wakati Mfumo wa HAKIMILIKI ambao
pia umetengenezwa
kwa teknolojia ya kisasa utafanya kazi ya kusajili wanachama wa COSOTA, kusajili kazi zao na kutoa leseni
za matumizi ya kazi za ubunifu.
Akizungumzia kuhusu mashindano ya Samia Taifa Cup Mkurugenzi wa Idara
ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Omary Singo amesema mashindano hayo yataaanzia katika ngazi ya kila mikoa ili
kupata timu bora na fainali zake zitafanyika jijini Dar es Salaam, Disemba 10 –
16, 2021 kwenye viwanja vya Benjamin Mkapa, Uhuru na Uwanja wa Ndani wa Taifa na
kwa kuanzia yatashirikisha michezo
mitatu ambayo ni Soka kwa wanaume na
wanawake, Netiboli kwa wanawake na Riadha kwa wanaume na wanawake
Singo ametoa wito kwa wadau wa michezo kuja kushuhudia michezo
hiyo ambapo amesema mashindano hayo yatahusisha pia mashindano ya fani anuai za
Sanaa hivyo kuleta hamasa na vionjo vya namna yake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni