Sifa za Mwalim bora ambaye atapata ajira haraka ni hizi hapa
Na Mwl Mikombe 0767000123
Namshukuru MwenyeziMungu Mmoja tu na wa Pekee anae endelea kunipa Uhai, Ndugu yangu, kumekuwa na wimbi kubwa la Waalimu mitaani na wengine wengi kulalamika kutolipwa mishahara kwa wakati au kamili
Pia kumekuwa na
malalamiko ya kutothaminiwa sehemu zao za kazi nakuonwa kuwa Ni waalimu wa kawaida
Wasio kuwa na mchango wowore
Hali hiyo
imenipelekea kuandika waraka huu ili wewe Mwalim ujitathmini je, wewe Ni Mwalim
bora au mbangaizaji?
Kabla ya kuanza
waraka huu naomba niwakumbushe, wamiliki kumlipa Mwalim au mtu ulie
muajiri kwa wakati ni haki yake na inafaida kubwa katika kuleta Ufanisi na
maendeleo ya Shule yako ya shule unayomiliki.
Pia ni Deni kubwa
usipo mlipa Mtumishi wako wakati akiwa hapa duniani, hakika utajuta
utakapotakiwa kumlipa mtumishi wako siku ya kiama huku wewe ukiwa huna kitu,
nakushauri walipe watumishi wako leo usije ukadaiwa siku ya kiama, kumbuka hicho
kidogo unacho walipa ndio kinaendesha maisha yao ya kila siku.
Utakubaliana na mimi
kuwa wafanyakazi wako wana watu wengine wengi wanawategemea hivyo
kumcheleweshea haki yake au kutomlipa Ni kumuadhibu yeye na familia
inayomtegemea. Kuwalipa wafanyakazi ni Dhulma iliyo kubwa.inayopaswa kuogopwa.
Baada ya kukumbusha
jambo hilo kwa wamiliki wa vituo, sasa naomba mniruhusu Twende kwenye mada,
hivi unafahamu nini maana ya mwalimu.
Mwalimu
ni Mtaalamu au Mjuzi anaejishughulisha kwa dhati Kuingiza Ujuzi, Maarifa,
Ufahamu au Utaalamu kwenye akili ya Mwana Adamu kwa kutumia Utaalamu, Nyenzo na
zana zinazostahiki ili kufikia Lengo analo litarajia.
Sifa
za Mwalim Bora…
Umeshawahi kujiuliza
sifa za Mwalim bora ni zipi, Mwalimu Bora anasifa 19 (kumi na Tisa), hizi hapa
1. Ni Mjuzi anae jifunza
Ni Lazima uwe
umesoma na kujua ulicho kisoma na unakiishi katika Maisha yako ya kila siku
lakini pia bado unaendelea kujifunza zaidi juu ya kile unachokijua hadi ifikie
Hatua kwenye Somo lako wewe Ni wakipekee kila mtu atamani wewe ndio
ufundishe.
2. Mbunifu na mwenye Athari
Mwalim Bora lazima
awe mbunifu wa namna ya kufundisha na kuelekeza pia kuonesha athari yake sehemu
alipo juu ya Anachokifundisha
Mfano, tunatarajia
shule Ina mwalim wa kingereza kwa kutazama Lugha ya Mawasiliano ya wanafunzi,
waalimu n.k. Pia inaenda hivyo hivyo kwa mwalim wa sayansi n.k. Kwamba
wakitafutwa waalimu wabunifu na wenye Athari wewe upo sio unakuwa mwalim kwa
muda wa Miaka 10 siku ukifukuzwa au kuondoka hakuna chochote ulicho acha Wala
hukumbukwi kwa chochote.
3. Mlezi
Mwalim lazima ajue
yeye ndio Mlezi anaechukua Jukumu la Mama au Baba, lazima Mwalim bora awe na
Programu maalumu za Ulezi kwa watoto wake mpaka uongozi wa Shule ukiri watoto
hawa Mwalim Fulani ndio mama yao kabisa na watoto wawe na raha kwa uwepo wako
yaani Mwalim sio awafuge watoto au awafanye wamuogope, hapana ispokuwa awapende
na wao wampende hadi ifikie hatua shida zao wawe tayari kuzieleza kwake.
Pia, kwenye Ulezi
Mwalim bora lazima awe na uhusiano wa karibu na wazazi kiwango ambacho wazazi
wa wanafunzi watambue Uwepo wako na wawe na furaha na matumaini kwa uwepo wako,
mwaimu Bora lazima ajue zile njia Tisa (9) za Malezi Bora kwa watoto.
4. Hobi na Furaha
Mwalim bora lazima
kazi ya Ualimu iwe imetoka moyoni mwake sio kwa sababu alifeli au alikosa kazi
fulani au anatafuta pesa Mwalim Bora ni yule ambae yupo tayari kutoa chochote
alichonacho kwa ajili ya Ufundishaji.
Ualim ndio kitu
pekee kinachompa furaha, kwake ualim ni kazi inayotoka moyoni na hayupo tayari
kuipoteza kwa gharama yoyote kwani hiyo ndio furaha yake na haoni raha kwa kazi
yoyote Ispokuwa Ualimu.
5. Mfanisi katika kazi zake
Mwalim bora hafanyi
kazi yake kwa hovyo, yeye ni Zaidi ya mfanisi, atahakikisha hakosi andalio la
Kazi, atahakikisha anajua idadi ya wanafunzi wake na uwezo wao kila mmoja na
mbinu za kuwasaidia ili wafanikiwe.
Pia nyaraka zote
anazijaza inavyostahiki sio Walim wa visingizio.
Mwl Bora Ni yule
Ambae hafanyi kazi sababu amemuona mkuu wa shule au kiongozi fulani yeye
hasukumwi kutekeleza majukumu yake pia yupo tayari kushika majukumu ya mwingine
kwa maslahi ya Shule na wanafunzi
wake.
Mwalim bora anaamini
majukumu yote ni yake na wengine wanamsaidia, Mwalim bora anaamini suala la
Kutangaza shule na kupata wanafunzi ni lake, hayupo tayari kufundisha wanafunzi
wachache hivyo yupo tayari kupita Mtaa kwa Mtaa au kwa njia yoyote kushiriki
upatikanaji wa wanafunzi.
Pia hayupo tayari
kuona mwanafunzi hata mmoja anaondoka atafanya kila hali kujaza wanafunzi na
kubuni mbinu na njia zozote asiondoke hata mwanafunzi mmoja.
Mwalimu Bora ndio
kiigizo Cha sifa njema na Maadili mema shuleni. Hafundishi sifa njema wala
Maadili mema kwa kutumia mdomo ispokuwa hufundisha sifa hizo kwa vitendo.
Wanafunzi na wafanyakazi
wanamuona anatenda tena anatenda kwa Ufanisi zaidi
Itaendelea…
Endelea kufuatilia
Makala za kielemu upate kuelimika hapa
Wewe kama Mwalim jichunguze
je, Sifa hizo Unazo Kama hauna chukua Hatua vinginevyo utaendelea kudai
mishahara kila Mwezi na kuhama shule moja mpaka miamoja .
Tukutane kwenye
awamu ya Pili kwa kumalizia sifa 19 za mwl Bora.
Nb: Malipo Bora na
kwa wakati yanatokana na Upekee wako yaani hapatikani kirahisi mtu Kama wewe.
Maoni 1
KIKUBWA ZAIDI KUELIMISHA JAMII HUSUSANI WAZAZI NA WALEZI
Chapisha Maoni