Waziri Mkuu azindua Vituo vya Huduma za Pamoja
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma za pamoja |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua
Vituo vya Huduma Pamoja (One Stop Centre Services) vya Shirika la Posta
Tanzania(TPC) na kuziagiza taasisi za umma ambazo hazijaanza kutumia huduma za
vituo hivyo kuanza kutoa huduma katika vituo vinavyopatikana ndani ya shirika
hilo katika mwaka wa fedha wa 2021/22.
Maagizo hayo ameyatoa leo jijini Dar es Salaam
katika Hafla ya uzinduzi wa vituo hivyo na kubainisha kuwa ni sehemu ya
utekelezaji ya Maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan inayoakisi Ilani ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 na kwamba lengo la Serikali kuona mchango wa
sekta ya habri mawasiliano unachangia uchumi pamoja na kuongeza ajira kwa
wananchi huku akizielekeza taasisi zinazotoa huduma kuweka vituo vya huduma
kwenye shirika hilo.
' Nazielkeza taasisi zinazotoa huduma zijiunge
na huduma hii Ofisi ya Rais na utumisi wa umma hakikisheni taasisi zote
zinajiunga na kuanza kutumia, vituo hivi vitasaidia watu kuinua vipato na
kuchocha maendeleo ya nchi," amesema Waziri Majaliwa.
Amezitaja baadhi ya taasisi hizo ni Kituo cha
Uwekezaji Nchini (TIC), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba,( TMDA ), Maeneo Maalum
kwa Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Tume ya Ajira na
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa
wingi kupata huduma hiyo katika vituo vilivyoanza kazi katika Ofisi Kuu
za Posta za Dar es Salaan na Dodoma kwani kufanya hivyo kutawapunguzia
msongamano katika ofisi za taasisi pamoja na kuokoa muda wa kupata huduma.
Amesisitiza kuwa kuanzishwa vituo hivyo ni
mageuzi makubwa ya shrika hilo lenye ofisi 350 nchi nzima hivyo na kwamba
vitawapunguzia wananchi changamoto ya kutembe ofisi ya taasisi zaidi ya moja
kufuata huduma.
Waziri Majaliwa amewasihi na kuwahimiza
watumishi wa shirika la posta kufanya kazi kwa weledi na kumpa ushirikiano
Kaimu Postamasta Mkuu ili wafikie malengo waliyojiwekea kuyatimiza.
Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndungulile ameishukuru Serikali kwa kutoa Sh
Bilioni 3.9 kwa ajili ya kuboresha shirika hilo kwa mfumo wa kidijitali na
kwamba watapokea fedha nyingine Sh Bilioni 3.9 ambazo zitakwenda kuboresha
mfumo huo.
Waziri Dkt. Ndungullile amesema wizara hiyo
imedhamiria kufanya mabadiliko ndani ya shirika hilo hasa kwa katika mwonekano
mpya, mwelekeo mpya lengo likiwa kuifanya posta kuwa kitovu cha biashara.
Pia amesema ifikapo mwaka 2025 kutakuwa na
dirisha moja lenye huduma za taasisi zote huku akiwaomba wanahabari na viongozi
wakawe mabalozi wa kuvitangaza vituo hivyo kwa jamii ifahamu kuwa posta
imeshaaza kutoa huduma ya vituo hivyo.
Naye Kaimu Postamasta Mkuu, Macrice Mbodo
amesema mradi wa vituo hivyo ni sehemu ya mradi ya Tanzania ya Kidijitali
na kwamba tayari Serikali imeshatenga Sh Bilioni 49.5 kuhakikisha unafika nchi
nzima.
Kaimu postamasta MKuu huyo amesema awamu ya
kwanza inahusisha vituo 10 katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha,
Mbeya, Morogoro, Tanga, Mwaza, Kigoma, Mjini Magharibi, na Pemba (Chake Chake).
Mbodo amebainisha awamu ya pili ya vituo hivyo
itaanza Januari 2023 na kukamilika mwezi Juni mwaka 2024 ukihusisha
kuuganishwa vituo 17 kwenye dirisha moja kwenye mikoa ya Pwani, Iringa, Songwe,
Rukwa,Njombe, Kilimanajro, Tabora, Lindi, Kagera, Simiyu, Manyara, Katavi na
Geita.
Pia amefafanua kuwa awamu ya tatu ya vituo vya
huduma pamoja itaanza mwezi Julai 2024 na kukamilika mwaa 2025 huduma zitakuwa
katika dirisha moja kuwasaidia wananchi kupata urahisi na kutopeteza muda.
Amezitaja huduma zilizoanza kutolewa katika
Vituo vya Dar es Salaam na Dodoma ni Utoaji wa Leseni za Biashara (TRA),
usajili wa vifo na vizazi (RITA), uhamiaji, usajili wa makampuni na majina ya
biashara (BRELA), Vitambulisho vya Taifa (NIDA), huduma za wastaafu (NSSF na
PSSF) pamoja na huduma za halmashauri.
Katika hatua nyingine amesema wanajipanga
kimkakati chini ya wizara husika kutelekeza vipaumbele vinne kuimarisha eneo la
usafirishaji wa mizigo na vifurushi, uwakala na uuzaji wa fedha, biashara mtandao
kupitia duka la mtandao na posta kiganjani iatakayotoa fursa kwa mteja kufahamu
mwenendo mzima wa mzigo wake.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na
Utawala Bora, Dkt. Francis Michael ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa
kuanzisha vituo hivyo kwani vitasaidia utaoji wa huduma kwa watja wa shirika la
posta na taasisi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundo Mbinu Selemani Kakoso ameiomba serikali kufuatilia deni la Sh Bilioni 3
la taasisi zinazodaiwa na posta zilipwe ili shirika liweze kusimama
kiundeshaji.
Katibu Mkuu -Umoja wa Posta Afrika, Sifundo
Moyo ameipongeza Serikali kwa kufanya maboresho ndani ya shirika hilo hsa posta
ya kidijitali hivyo umoja huo utaendelea kushirikiana na Posta.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla
amempongeza Mbodo kwa uanzishaji wa huduma za vituo hivyo na kubainisha kuwa
vimekuja wakati mwafaka hivyo ofisi ya mkoa itatoa ushirikiano kuhakikisha
vinafanya kazi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni