Jaji Mutungi, IGP kukutana na wadau wa vyama vya siasa.
Na Mussa Augustine.
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imesema kuwa itaitisha mkutano na Jeshi la Polisi Nchini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa ili kuondoa kujadili namna ya kuondoa migogoro inayotokea baina ya Wanasiasa na Polisi wakati wa makongamano yao ya Kisiasa.
Msajili wa vyama vya siasa Nchini Jaji Frances Mutungi akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo mkoani Dar es salaam. |
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Msajili wa vyama vya siasa Nchini Jaji Frances Mutungi amesema kwamba tayari ofisi yake imeshakutana na IGP nakukubaliana kuitisha mkutano wa wadau ili kujadili na kuondoa mivutano ya Polisi na Vyama vya Siasa.
“Kikao hicho kitafanyika hivi karibuni mara baada ya taratibu kukamilika,hatujakilia hii hali inaleta tahaluki fulani kwenye jamii kwani mikutano ya ndani ,makongamano yakisiasa imekua mtazamo hasi kuona kila mkutano au kongamano polisi wanazuia “alisem Jaji Mutungi.
Aidha Msajili huyo wa vyama vya siasa amesema kwamba “msajili wa vyama vya siasa ni mlezi wa vyama vya siasa na nimsimamizi wa sheria ya vyama vya siasa ,hivyo sisi hatujafikia kuona siasa za taharuki, hivyo naweza kutumia neno linalotumika kwamba hakuna Sintofahamu" hivyo lengo letu ni kuondoa hali hii ya mvutano" amesema
Amesema kwamba wanasiasa ni wasikivu wana uchungu na nchi vivyo hivyo vyombo vya Usalama vina Uchungu na nchi , hivyo tunataka tuondoe dhana kwamba vyama vya siasa vimekosea hapa, polisi wamekosea hapa, sisi ni watu wazima kwanini tusikutane tuyamalize” Ameongeza.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamefurahishwa na hatua hiyo huku wakisisitiza kwamba itasaidia kuondoa mutano baina yao na jeshi la Polisi Nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni