Zinazobamba

Sifa za Mwalim bora ambaye atapata ajira haraka ni hizi hapa

 



Na Mwl Mikombe 0767000123

 Namshukuru MwenyeziMungu Mmoja tu na wa Pekee anae endelea kunipa Uhai, Ndugu yangu, kumekuwa na wimbi kubwa la Waalimu mitaani na wengine wengi kulalamika kutolipwa mishahara kwa wakati au kamili

Pia kumekuwa na malalamiko ya kutothaminiwa sehemu zao za kazi nakuonwa kuwa Ni waalimu wa kawaida Wasio kuwa na mchango wowore

Hali hiyo imenipelekea kuandika waraka huu ili wewe Mwalim ujitathmini je, wewe Ni Mwalim bora au mbangaizaji?

 

Kabla ya kuanza waraka huu naomba niwakumbushe, wamiliki  kumlipa Mwalim au mtu ulie muajiri kwa wakati ni haki yake na inafaida kubwa katika kuleta Ufanisi na maendeleo ya Shule yako ya shule unayomiliki.

Pia ni Deni kubwa usipo mlipa Mtumishi wako wakati akiwa hapa duniani, hakika utajuta utakapotakiwa kumlipa mtumishi wako siku ya kiama huku wewe ukiwa huna kitu, nakushauri walipe watumishi wako leo usije ukadaiwa siku ya kiama, kumbuka hicho kidogo unacho walipa ndio kinaendesha maisha yao ya kila siku.

 

Utakubaliana na mimi kuwa wafanyakazi wako wana watu wengine  wengi wanawategemea hivyo kumcheleweshea haki yake au kutomlipa Ni kumuadhibu yeye na familia inayomtegemea. Kuwalipa wafanyakazi ni Dhulma iliyo kubwa.inayopaswa kuogopwa.

 

Baada ya kukumbusha jambo hilo kwa wamiliki wa vituo, sasa naomba mniruhusu Twende kwenye mada, hivi unafahamu nini maana ya mwalimu.

Mwalimu ni Mtaalamu au Mjuzi anaejishughulisha kwa dhati Kuingiza Ujuzi, Maarifa, Ufahamu au Utaalamu kwenye akili ya Mwana Adamu kwa kutumia Utaalamu, Nyenzo na zana zinazostahiki ili kufikia Lengo analo litarajia.

Sifa za Mwalim Bora…

 

Umeshawahi kujiuliza sifa za Mwalim bora ni zipi, Mwalimu Bora anasifa 19 (kumi na Tisa), hizi hapa

 

1.  Ni Mjuzi anae jifunza

Ni Lazima uwe umesoma na kujua ulicho kisoma na unakiishi katika Maisha yako ya kila siku lakini pia bado unaendelea kujifunza zaidi juu ya kile unachokijua hadi ifikie Hatua kwenye Somo lako  wewe Ni wakipekee kila mtu atamani wewe ndio ufundishe.

 

 

2.  Mbunifu na mwenye Athari

Mwalim Bora lazima awe mbunifu wa namna ya kufundisha na kuelekeza pia kuonesha athari yake sehemu alipo juu ya Anachokifundisha

Mfano, tunatarajia shule Ina mwalim wa kingereza kwa kutazama Lugha ya Mawasiliano ya wanafunzi, waalimu n.k. Pia inaenda hivyo hivyo kwa mwalim wa sayansi n.k. Kwamba wakitafutwa waalimu wabunifu na wenye Athari wewe upo sio unakuwa mwalim kwa muda wa Miaka 10 siku ukifukuzwa au kuondoka hakuna chochote ulicho acha Wala hukumbukwi kwa chochote.

 

3.    Mlezi

Mwalim lazima ajue yeye ndio Mlezi anaechukua Jukumu la Mama au Baba, lazima Mwalim bora awe na Programu maalumu za Ulezi kwa watoto wake mpaka uongozi wa Shule ukiri watoto hawa Mwalim Fulani ndio mama yao kabisa na watoto wawe na raha kwa uwepo wako yaani Mwalim sio awafuge watoto au awafanye wamuogope, hapana ispokuwa awapende na wao wampende hadi ifikie hatua shida zao wawe tayari kuzieleza kwake.

Pia, kwenye Ulezi Mwalim bora lazima awe na uhusiano wa karibu na wazazi kiwango ambacho wazazi wa wanafunzi watambue Uwepo wako na wawe na furaha na matumaini kwa uwepo wako,  mwaimu Bora lazima ajue  zile njia Tisa (9) za Malezi Bora kwa watoto.

 

4.  Hobi na Furaha

Mwalim bora lazima kazi ya Ualimu iwe imetoka moyoni mwake sio kwa sababu alifeli au alikosa kazi fulani au anatafuta pesa Mwalim Bora ni yule ambae yupo tayari kutoa chochote alichonacho kwa ajili ya Ufundishaji.

Ualim ndio kitu pekee kinachompa furaha, kwake ualim ni kazi inayotoka moyoni na hayupo tayari kuipoteza kwa gharama yoyote kwani hiyo ndio furaha yake na haoni raha kwa kazi yoyote Ispokuwa Ualimu.

 

5.  Mfanisi katika kazi zake

Mwalim bora hafanyi kazi yake kwa hovyo, yeye ni Zaidi ya mfanisi, atahakikisha hakosi andalio la Kazi, atahakikisha anajua idadi ya wanafunzi wake na uwezo wao kila mmoja na mbinu za kuwasaidia ili wafanikiwe.

Pia nyaraka zote anazijaza inavyostahiki sio Walim wa visingizio.

Mwl Bora Ni yule Ambae hafanyi kazi sababu amemuona mkuu wa shule au kiongozi fulani yeye hasukumwi kutekeleza majukumu yake pia yupo tayari kushika majukumu ya mwingine kwa maslahi ya Shule na wanafunzi wake.

Mwalim bora anaamini majukumu yote ni yake na wengine wanamsaidia, Mwalim bora anaamini suala la Kutangaza shule na kupata wanafunzi ni lake, hayupo tayari kufundisha wanafunzi wachache hivyo yupo tayari kupita Mtaa kwa Mtaa au kwa njia yoyote kushiriki upatikanaji wa wanafunzi.

 

Pia hayupo tayari kuona mwanafunzi hata mmoja anaondoka atafanya kila hali kujaza wanafunzi na kubuni mbinu na njia zozote asiondoke hata mwanafunzi mmoja.

 

Mwalimu Bora ndio kiigizo Cha sifa njema na Maadili mema shuleni. Hafundishi sifa njema wala Maadili mema kwa kutumia mdomo ispokuwa hufundisha sifa hizo kwa vitendo.

Wanafunzi na wafanyakazi wanamuona anatenda tena anatenda kwa Ufanisi zaidi

Itaendelea…

Endelea kufuatilia Makala za kielemu upate kuelimika hapa

 

Wewe kama Mwalim jichunguze je, Sifa hizo Unazo Kama hauna chukua Hatua vinginevyo utaendelea kudai mishahara kila Mwezi na kuhama shule moja mpaka miamoja .

Tukutane kwenye awamu ya Pili kwa kumalizia sifa 19 za mwl Bora.

Nb: Malipo Bora na kwa wakati yanatokana na Upekee wako yaani hapatikani kirahisi mtu Kama wewe.

Maoni 1

Bila jina alisema ...

KIKUBWA ZAIDI KUELIMISHA JAMII HUSUSANI WAZAZI NA WALEZI