Miaka sita ya Mufti Zubeir (Septemba 10, 2015-2021)… · JUVIKIBA waja na wiki ya Mufti Zubeir
Katika kusheherekea miaka sita ya utumishi wa Mufti na Sheikh Mkuu
wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Septemba 10, 2021, Jumuiya ya vijana wa Kiislam
Bakwata (JUVIKIBA) wameandaa hafla kubwa itakayodumu kwa wiki moja yenye
dhamira ya kumpongeza kwa kutimiza miaka sita utumishi wake lakini pili
kupongeza kazi kubwa aliyofanya ndani ya muda huo
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Bakwata,
Mwenyekiti wa Jumiya hiyo, Muharam Khamis Pembe amesema tayari maandalizi kwa
ajili ya wiki ya Mufti yanaendelea.
Sheikh Pembe amesema Wiki ya Mufti itakuwa na mambo mengi na
kwamba itaanza rasmi Septemba 6, 2021 na kukamilika kwake Septemba 12, 2021,
ambapo ndani ya wiki hiyo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwamo mchezo wa
mpira wa miguu.
Shughuli zingine ni pamoja na kutembelea wagonjwa mahosptalini,
kuendesha mashindano ya quran, kuwasomea dua waliotangulia mbele za haki,
kufanya usafi wa mazingira, Mufti wa Tanzania kula na watoto yatima pamoja na
kutembelea magerezani ili kuwaona ndugu jamaa na marafiki wenye shida
mbalimbali.
Sheikh Pembe amesema mbali na kwenda katika magereza lakini pia
wanakusudia kufika Soba House ili kuwaombea dua watu wa kule waondokane na
matatizo yao, warejee majumbani kuendesha familia zao.
Akizungumzia kuhusu Muendelezo wa siku hiyo ya Mufti, Sheikh Pembe
alisema wamepanga kila mwaka kuwe na tukio hilo kwani wanadhani itasaidia sana
kumtia moyo Mufti kwa kazi kubwa anazofanya.
“Siku ya Mufti Day itakuwa Septemba 10, 2021, septemba 12 tutakuwa
na hitimisho ambapo kutakuwa na mchezo wa mpira wa miguu kati ya JUVIKIBA Makao
Makuu na Timu ya Sheikh wa Mkoa wa wa Dar es salaam, mshindi katika mchezo huo
ataibuka na kikombe cha Mufti,” alisema
Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka sitaSheikh
Pembe amesema Mufti ameweza kuweka makaadhi nchi nzima, ambao mpaka sasa
wanafanya kazi nzuri ya kuwasaidia waislam katika changamoto mbalimbali za
kudai haki zao hasa katika masuala ya ndoa.
Mafanikio mengine ni pamoja na kutengeneza baraza jipya na la
kisasa lenye malengo mazuri na waislam, sasa hivi bakawata imebadilika baada ya
kuweka viongozi wenye weledi
“Amejitahidi kutengeneza katiba ya Bakwata, ukiisoma katiba hiyo kifungu
cha 103 ambacho kinamahusiano na taasisi zingine, Mufti ameifanyia kazi
kipengele hicho kwa vitendo,” aliongeza.
Amesema Mufti Abubakar amejitahidi katika kujenga umoja miongoni
mwa taasisi, watu wote ni shahidi, amekuwa akifanya kazi na taasisi zote
akiamini Bakwata ndio taasisi mama hapa nchini.
Pia ameanzisha bodi ya wadhamini, bodi hiyo kwa sasa ipo chini ya
aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Kamanda
Suleiman Kova, inafanya kazi kubwa na wengi wanaifurahia
Bakwata imeanza kuaminiwa na kukubaka na waislam wengi kiasi
ambacho wengi wanatamani kufanya nayo kazi.
“Kwa kweli mafanikio ni mengi, katika kipindi chake tumeshuhudia
msikiti mkubwa Tanzania, msikiti ule unao uwezo wa kuchukua watu 10,000 kwa
mara moja,” alisema.
Mbali na ushirikiano na taasisi zingine za kidini pia Bakwata
imefanikiwa katika kuwandaa viongozi wake kushiriki kutengeneza amani ya nchi
ya Tanzania, hivi sasa kila mkoa una kamati za amani ambazo zinafanya kazi
kubwa ya kudumisha amani.
Kauli mbiu ya wiki ya Mufti ni Tumekuamini,
kazi inaonekana na tunatarajia sababu ya kuja na kauli mbiu hiyo ni
kutokana na kazi alizofanya, ameweza na tunataraji atafanya Zaidi.
Aidha Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa baraza la vijana wa mikoa
kuazimisha siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali na kuwaomba masheikh wa
mikoa kuwapa ushirikiano vijana kutuimiza majukumu yao
Ends,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni