Chuo Kikuu Zanzibar chawaita wazazi viwanja vya mnazi mmoja, Dkt Salma asema chuo chao ni bora
Hussein
Ndubikile, Dar es Salaam
Chuo
Kikuu cha Zanzibar (Zu) kimewakaribisha na kuwashauri wazazi wenye watoto
waliomaliza Kidato cha nne, sita, ngazi za cheti, astashahada na shahada
kuhudhuria katika banda lao la Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia
ili wapatiwe elimu ya orodha ya kozi zinazofundishwa na walimu na
wataalamu wa idara waliobobea.
Hayo
yamesemwa na Mhadhiri wa Chuo hicho katika Idara ya Biashara- Kitengo cha
Uhasibu na Fedha, Dkt. Salama Yusuf kwenye maonesho hayo yanayoendelea Katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema
wazazi watakaofika katika banda lao watapata fursa ya kupewa elimu ya kozi
zinazowafaa kusoma watoto wao kulingana na ufaulu walionao kutoka kwa walimu na
wataalamu wa idara waliopo hapo na kwamba chuo hicho kina mazingira bora ya
kujisomea.
"
Wazazi wahudhurie hapa bandani watapatiwa elimu sahihi ya kozi tutoazo
zinazowafaa watoto wao tuna walimu na wataalamu waliobobea tuna mazingira bora
ya kujisomea watapohitimu watatoka wakiwa mahiri katika taaluma
walizosomea," amesema Dkt. Salama.
Amebainsha
kuwa katika kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu chuo
hicho kimeanzisha kozi ya ujasiriamali katika ngazi ya cheti na shahada
kuwasaidia wahitimu kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.
Amesisitiza
kuwa chuo kinazingatia kanuni na miongozo ya wizara ya afya kwani katika maeneo
ya chuo hicho kilichopo Tunguu nje ya Mji wa Zanzibar wanafunzi, walimu
na wakuu wa idara wanavaa Barakoa, upakaji vitakasa mikono, ukaaji wa mita moja
madarasani pamoja na meneo mengine.
Ameipongeza
TCU kwa kuendelea kuandaa maonesho hayo kwani yanatoa fursa adhimu kwa vyuo
vikuu na taasisi kujitangaza na utoaji elimu kwa wanafunzi wanaofnaya udahili
wa masomo wa mwaka 2021/22 huku akiishauri tume hiyo kuboresha mfumo wa mtandao
wake ili ufanye kazi kwa haraka.
Dkt.
Salama amezitaja kozi mbalimbali zinazofundishwa na chuo hicho katika ngazi
mbalimbali ikiwemo Usimamizi wa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Sheria, Biashara
ya Teknolojia, Ustawi wa Jamii, Uuguzi na Ukunga, Ushauri wa Saikolojia,
Masoko, Uhasibu, Sayansi katika Uuguzi,Utawala pamoja na Sanaa katika
Uchumi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni