Chuo Kikuu Iringa chaeleza utofauti wao na vyuo vingine Tanzania, washauri wanafunzi kujiunga nacho
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Iringa (uoi)
kimewakaribisha wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mwaka wa
masomo wa 2021/22 kwani watafaidika na kozi mbalimbali ikiwemo ya Shahada ya
Masoko na Ujasiriamali itakayowasaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa
kuanzisha kampuni zao baada ya kuhitimu masomo yao chuoni hapo.
Hayo yamesemwa na Mhadhiri wa Chuo
hicho Angel Ezekiel katika Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na
Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini(TCU) yanayondelea kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema katika kukabiliana na
tatizo hilo wamejipanga kufundisha kozi kwa nadharia na vitendo ili kutengeneza
kundi kubwa la wahitimu wanaoweza kulimudu tatizo la ajira hapa nchini kwani
wataweza kuanzisha kampuni zao wenyewe.
" Tunachanganya nadharia na
vitendo kuendana na soko la ajira wanafunzi watakaojiunga nasi watamaliza
masomo yao wakiwa wanaweza kujiajiri Barani Afrika ndio chuo kipekee
kinachofundisha kwa vitendo masuala ya biashara na ujasiriamali" amesema
Angel.
Amebainisha kuwa kupitia shahada
hiyo wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo watapata fursa ya kufundishwa jinsi
ya kuanzisha biashara chini ya usimamizi wa walimu waliobobea hivyo mara
watakapohitimu wataendelea nazo.
Ameongeza kuwa wanafunzi
watakaosoma taaluma ya Uhandishi wa Habari watafundishwa katika mazingira ya
nadharia na vitendo katika matukio yanayofanyika uoi kwani chuoni hapo kuna
radio ya Hope Fm, Gazeti la chuo pamoja na Tv.
Amesisitiza kuwa chuo hicho
kinafundisha kozi mbalimbali katika ngazi ya Cheti, Astashahada, Shahada na
Shahada ikiwemo Uhandishi wa Habari, Sheria, Mendeleo ya Jamii, Usimamizi wa
Biashara, Ualimu, Utawala, Masoko, Utafiti, Manunuzi, Utalii, Kompyuta pamoja
na uchungaji.
Maonesho hayo yalizinduliwa Julai
27 mwaka huu katika viwanja hivyo na Baraza la Mapinduzi na Kiongozi na Katibu
Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Mhandisi, Zena Ahmed Said na yanatarajiwa kufikia
tamati Julai 31, 2021.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni