Zinazobamba

DC Ilala asifu kituo cha kulelea yatima Kigamboni

 


Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija akizungumza na waandishi wa habari katika Tamasha la usiku wa Amani lililofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel Ilala Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa kituo hicho Hajat Zubeda Abdallah





Na mwandishi wetu

Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amesifu ulezi unaofanywa na kituo chawatoto yatima cha Amani Foundation chenye makao makuu yake Kibugumo wilaya ya kigamboni, jijini Dar es salaam.

Aidha Ludigija ameahidi kutoa ushirikiano katika kituo hicho kwani kimethibitisha kuwa hawako kwa ajili ya maslahi binafsi bali kusaidia watoto kufikia ndoto zao.

Akizungumza jiji Dar es salam katika tamasha maalum la usiku wa amani Foundation, Ludigija amesema amewahi kuhudhuria hafla za watoto mayatima nyingi lakini amani foundation wako tofauti na wengine, wenyewe wanawajali watoto jambo ambalo limesababisha vijana kuonekana wenye nuru katika nyuso zao.

Ludigija ambaye alionekana mwenye furaha kuhudhuria hafla hiyo ambayo ilikuwa na  dhamira ya kuwafanya watoto wafurahi amesema ulezi wa amani foundation ni wa kiwango cha juu na ni mfano kwa vituo vingine.

“Nimeambiwa hapa mbali ya kulea yatima lakini pia mnalea vipaji vya watoto hawa, Kwa muda mchache ambao nimefika hapa nimegundua mko tofauti na wengine, vijana wenu wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika masuala ya kusifu kupia kaswida zao,

Kunatofauti kubwa kati ya vituo vingine na chenu, sina maana ya kuviponda vingine hapana ila nazungumza kweli, nyie mnafanya kazi kubwa na watoto wanaonekana wanafuraha,” alisema Ludigija.

Aidha ametoa wito kwa vituo vingine kujitahidi kuifanya kazi ya kulea yatima kwa ikhlas, kwani hiyo ni kazi ya kitume, na inayohitaji kujitoa Zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani Foundation, Hajat Zubeida Abdallah amesema kituo chake kina utaratibu wa kuandaa matamasha ili kukutana na wadau kuona vipaji vya yatima lakini pia kupata msaada kutoka kwao.

“Sisi huwa tunaendesha matamasha kama haya kila mwaka, dhamira yetu ni kuwapa furaha watoto, wasione wako wapweke, tunachagua eneno tunakula nao chakula, wanafurahi basi,” alisema

Aidha akizungumzia historia ya kituo hicho, kituo chao licha ya kwamba kina umri mdogo lakini kimeweza kuaminika na jamii kiasi ambacho wapo wadau waliojitolea kuwajengea nyumba.

Amesema kituo kilianza na watoto 4, lakini hadi sasa kina watoto 54 ambao kati yao wapo wanaoishi kituoni na wengine wanaendelea na masomo katika shule za bweni (Boarding).

Kwa upande wake mmoja wa wafadhili wa kituo hicho Hajat Safia Abedi Salum Hafsi ameelezea kufurahishwa kwake na uongozi wa Hajat Zubeida kwani umenyooka na hauna makandokando.

Amesema wao wamekuwa na kituo hicho kwa muda mrefu sasa hawajaona ubadhirifu wowote kitu ambacho kimewavutia kuendelea kuwafadhili.

“Mimi ni mdau wa kituo hiki, ni mmoja wa wafadhili, tuko nao hawa watoto kwa kila hali, hatujawahi kuwaacha peke yao, tunamuomba Allah atuongoze kufanya heri hizi,” alisema

Aidha ametoa wito kwa umma kufika katika kituo hicho kujionea vipaji vya watoto, amesisitiza kuwa ukifika kituoni hapo utajisikia moyo umepoa, watoto wanasoma dua vizuri, hajawahi mtu akasomewa dua akaondoka anasikitika, ni watoto ambao wanakubuli za ajabu.

Kituo cha amani foundation for orphanage ni moja ya kituo kikubwa kwa sasa kilichopo kigamboni, kilianza kazi yake mwaka 2014 kikiwa na watoto 4, sasa hivi wana watoto 54.


Hakuna maoni