Udugu Social Help welfare yawafariji mayatima Mbagala
Taasisi ya Udugu
Social Help Welfare yenye Makao Makuu yake Buguruni Jijini Dar es Salaam imefanikisha
nia yake ya kuwafariji mayatima wa kituo cha Al-Azim kilichopo Mbagala kwa kujumuika
nao na kupata chakula cha pamoja.
Aidha Taasisi hiyo
imetoa wito kwa wadau kuendelea kuwakumbuka na kuwajali mayatima na watoto
wanaoishi katika mazingira magumu popote pale walipo kwani bado wanazo
changamoto nyingi zinazohitaji ufumbuzi.
Akizungumza mara
baada ya kupata chakula cha mchana na mayatima, mratibu wa kundi hilo lenye
wanachama Zaidi ya 20, Hajat Neema Maumba amesema kilichowasukuma kushiriki
chakula pamoja na mayatima ni kuwafariji, wasijione wapweke katika maisha yao.
Amesema ni utaratibu
wao wa kila mwaka kushiriki chakula na watoto yatima na wamekuwa wakifanya
hivyo katika maeneno mbalimbali katika jiji la Dar es salaam.
Amesema taasisi yao
ya Udugu Social Help welfare sio ya kidini na lakini wengi wao ni waislam, wanasaidia
watu mbalimbali bila kujali dini zao.
“Sisi tunaitwa Udugu
Social Help welfare, Makao makuu yetu yapo Buguruni Malapa, tuko wakina mama
20, tulianza kazi mwaka 2009, tumefanya kazi sehemu nyingi na bado
tunaendelea,” alisema
Tumesikia majonzi
mengi baada ya watoto kueleza changamoto zao, tunamuomba mwenyezi Mungu
atuafikishe sisi na wengine tuweze kusaidiana, yatima sio mtoto wa mtu mmoja,
ni watoto wetu, kama alivyosema Mtume wetu Muhammad (saw) kwamba katika nyumba
yenye yatima wakalala njaa na nyumba nyingine wakala basi watu wote katika mtaa
huo wanapata dhambi,” aliongeza
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa taasisi ya kulelea watoto yatima na wenye mazingira hatarishi
cha Al-Azam Orphanage center Sheikh Musa Chele ametoa wito kwa wafadhili kuacha
kuwatumia watu wa kati kufikisha sadaka zao katika makao ya watoto yuatima.
Amesema kwa muda
mrefu watu hao wa kati (agent) wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya kwa
kujinufaisha wao wenyewe badala ya watoto mayatima.
Ametoa mfano katika
kituo chake pekee jumla ya milioni 80 zimeliwa na watu wa kati jambo ambalo
lina muudhi sana na kuamua kulitolea ufafanuzi.
Aidha akielezea
historia ya kituo chao, Sheikh Musaa alisema Kituo chao kimeanzishwa mwaka 2009
kikiwa na watoto 10, wavulana 5 na wasichana 5, hadi kufika mwaka 2021,
walikuwa na watoto 60, kati yao wanawake 35 na wanaume 25, aidha kati ya watoto
60, 45 wanaishi katika kituo na wengine wanalelewa wakiwa majumbani mwao.
Amesema Kituo
kinakabiliwa na changamoto nyingi, lakini kubwa ni huduma za afya, watoto wengi
hawana bima za afya ili kuwasaidia kupata matibabu bila hofu.
Pia amesema kuna
changamoto ya rasilimali fedha za kulipa pango la nyumba, ada za wanafunzi, na
chakula, kwa mwezi wanalipa shilingi
300,000 fedha ambazo ni nyingi kwa uwezo wao.
Aidha kwenye upande wa
mafanikio kituo kimeweza kununua kiwanja na kuwaomba wadau kuwajengea nyumba
ili watoto wakaishi huko na kuepukana na adha ya kupanga.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni