Zinazobamba

TBC yasaini Mkataba wa Sh Bilioni 3.54 na TFF kutangaza Mechi za Ligi Kuu Bara Redioni

 



Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesaini Mkataba wa Haki za Matangaza ya kutangaza Mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara redioni wenye thamani ya Sh Bilioni 3.54 na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Mratibu wa Miradi na Masoko wa shirika hilo, Gabriel Nderumaki amesema wameamua kusaini mkataba kuendelea kuipa hadhi na thamani ligi pamoja na kuvisaidia vilabu kuviondolea changamoto katika mashindano hayo.

Amebainisha kuwa  TBC wameiona fursa ya kutangaza ligi hiyo lengo likiwa kuipaisha ifike kuwa miongoni mwa ligi bora na kwamba uingiaji mkataba huo ni chachu ya maendeleo ya soka katika Mashindano ya Ligi hiyo.

Kwa upande wake Rais wa TFF , Wallace Karia amelishukuru shirika hilo kwa kuonyesha ni kwa jinsi linatambua umuhimu pamoja na dhamira ya kuendelea kuipa thamani ligi kuu  na kwamba mkataba utasaidia kupunguza changamoto za vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo.

" Miaka nyuma suala halikuwepo ila kwa sasa inaonyesha jinsi ligi yetu inavyoendelea kupanda thamani siku hadi siku mkataba huu ni ukombozi kwa vilabu katika kuvipunguzia makali ya uendeshaji wakati wa mashindano," amesema Karia.

Amesisitiza kuwa wakati TFF inaanza utiaji mikataba ya kuipa thamani ligi vilabu vishiriki vilikuwa vipkipatiwa Sh Milioni saba ikaongezeka kwa udahamini wa matangazo ya Televisheni kufikia Sh milioni 100 na kwamba kwa msimu ujao utafiki Sh mil 400.

Ameongeza kuwa mkataba huo hauzizuii redio nyingine kutangaza ligi hiyo bali zinatakiwa kuingia makubaliano na TBC lenye mkataba wa kutangaza matangazo redioni na kukazia duniani kote mkataba wa aina husainiwa kwa nuda mrefu sababu mwekezaji hununua mitambo mipya hivyo huhitaji kurudisha gharama na kupata faida.
 
Amefafanua kuwa TFF limeanza kupata fedha kupitia mitandao yake ikiwemo Runinga ya Ligi kuu pamoja na mitandao ya kijamii ya Instagram, na kubainisha fedha zinakuja kutokana shirikisho kuwa imara kiutendaji.

Naye Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi amelishukuru TBC na kusema mkataba huo utatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka kwa kuifanya ligi kuwa bora na yenye thamani.

Mwenyekiti wa Klabu ya Mbeya City, Venance Msolla amesema ili vilabu viwe bora na viweze kujiendesha  vinahitaji benchi bora la ufaundi, usajili wa wachezaji wazuri na kwamba mkataba utazisaidia timu za mikoani kuondokana na changamoto za kiundeshaji.

Hakuna maoni