ussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya wanachama wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wanaopanga kufanya maandamano badala yake wasubiri uamuzi wa Mahakama utakaotelewa dhidi ya kesi inayomkabili Mwenyekiti chama hicho kitaifa, Freeman Mbowe.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam alisema wanachama wa CHADEMA wanapaswa kuelewa mwenyekiti wao si malaika bali ni binadamu anayeweza kutenda kosa la uhalifu na kwamba kufanya maandamano ni kuvunja sheria hivyo wanatakiwa kusubiri mahakama itoe uamuzi.
" Wanachama wajue Mbowe si Malaika ni binadamu anayeweza kufanya uhalifu kama ni mkweli anamwogopa Mungu waende kumuuliza atawaeleza ukweli," amesema IGP Sirro.
Amebainisha mwaka jana kabla Uchaguzi Mkuu aliweka wazi kuna watu wanapanga njama za kulipua visima vya mafuta pamoja na kufanya mauaji ya viongozi na kusisitiza kuwashughulikia kabla hwajafanya matukio hayo hivyo tayari jeshi hilo limeshawasilisha ushahidi kinachosuburiwa mahakama itoe uamuzi.
Ameongeza kuwa polisi hawamwonei Mbowe bali linafuata sheria kwa watu wanaotaka kuharibu amani na utulivu kwa manufaa yao na kuzikosoa asaki za kiraia na viongozi wa dini wanaosema mwanasiasa huyo anaonewa.
Amefafanua kuwa jeshi hilo haliwezi kuwaacha watu wachache wafanye nchi isikalike kwa kuendekeza tamaa zao na kwamba watakaokaidi utii wa sheria watachukuliwa hatua.
Aidha, amewaonya watu kutoka mikoani walioandaliwa kufanya maandamano kutofanya hivyo kwani polisi halitawavumivilia kwa kuwashughulikia kikamilifu.
Katika hatua nyingine, IGP Sirro ametoa maagizo kwa makamanda wote wa mikoa kufanya oparesheni ya mwezi mmoja ya kuwakamata na kuwachukulia hatua madereva Bodaboda wanaokiuka sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwemo kutovaa kofia (Helmet), kupakia mishkaki pamoja na abiria kutopewa kovia.
Amesema wameshajitahidi kutoa elimu kwa madereva hao ila kuna baadhi wasiotii sheria kusababisha ajali nyingi kutokea hivi karibuni.
Wakati huo huo, ameziomba halmashauri kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana watu wanaokataa kuchangia fedha za ulinzi shirikishi na kuzipongeza halmashauri ya Ubungo na Kinondoni kwa kuwa na sheria hizo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni