Zinazobamba

SANGENI INTERNATIONAL KINARA WA UTOAJI WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU NJE YA NCHI.

Na Mussa Augustine

Sangeni International ambao ni wakala wa elimu ya juu nje ya nchi imejipambanua kuendelea kutoa huduma bora kwa wanafunzi watakaotaka kwenda kusoma elimu ya juu nje ya nchi kupitia kampuni hiyo.

Meneja Mkuu Jadian Saimon wa wakala wa kuwatafutia nafasi za masomo wanafunzi  nje ya nchi Sangeni International, akielezea huduma wanazozitoa kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) waliotembelea banda hilo katika maonesho ya 16 ya elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia mkoani Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  maonesho ya 16 ya vyuo vikuu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam,yakiwa  chini ya uratibu wa Tume ya Vyuo vikuu Nchini (TCU) Meneja Mkuu wa Wakala huo Bw. Jadian Saimon alisema kwamba Sangeni Inaternational inawasaidia wanafunzi wanatazania kusoma nje ya nchi na kutimiza ndoto zao.

Bw. Saimon aliendelea kuwaambia wanahabari kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikiwaunganisha wanafunzi raia wa Tanzania na vyuo mbali mbali duniani hususani vyuo ambavyo vianatoa  kutoa ofa za punguzo la ada hadi asilimia 50 na zenye uhusiano na vyuo vikuu vya nchini India nakutumia fursa hiyo kuwataka wazazi au walezi kuchangamkia fursa hiyo katika kipindi hiki cha udahili wa wanafunzi wa kujiunga na elimu ya juu.

“Katika Maonesho haya ya 16 ya Elimu ya Vyuo Vikuu 2021 yanayofanyika kuanzia Julai 26 mpaka Julai 31 Julai katika viwanja hivi vya Mnazi Mmoja, Sangeni International ikishirikiana na MANIPAL ACADEMY of HIGHER EDUCATION DUBAI CAMPUS kupitia shughuli hii ya maonesho chuo kinatoa punguzo la ada ya mwaka asilimia 30 kwa wanafunzi mwaka wa kwanza na asilimia 25 kwa digrii ya pili wale tu watakaojisajili na chuo. “ alisema Meneja huyo.

Huduma zikiendelea katika banda la wakala wa kuwatafutia nafasi za masomo wanafunzi  nje ya nchi Sangeni International, katika maonesho 16 Elimu ya juu ya Sayansi na Teknolojia Mnazi Mmoja mkoani Dar es salaam.

Nakuongeza kwamba “Wanafunzi hao pia watapata tiketi ya ndege kuelekea mji wa Dubai na watapokelewa uwanja wa ndege na kufikishwa kwenye malazi ya chuo na watalipiwa bima ya afya kubwa kwa mwaka wa kimasomo wa mwanzo”.

Bw. Saimoni aliendelea kuzungumza  kwamba Sangeni International  inahakikisha  inashirikiana na chuo  kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata kazi za muda za kulipwa wakati wakiwa masomoni Dubai kwa kuwakabidhi vibali au vyeti vya “No Object Certificate” (NOC) hivyo hali hiyo itawasaidia wanafunzi kupata kipato cha kujikimu kipindi cha masomo yao.


Hakuna maoni