Zinazobamba

Wanafunzi NIT wahusiwa kujiajiri

 








 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Eng. Prof. Sillvester Mpanduji amewashauri wahitimu wa chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) kuangalia fursa mbalimbali za kujiajiri na kwamba Sido ipo tayari kuwasaidia kitaalamu hasa pale wanapokabiliwa na changamoto za kiutendaji

Akizungumza katika hafla ya convocation inayotumika kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri chuoni hapo alisema wanafunzi wasifikilie kuajiliwa tu badala yake wajikite kuangalia jinsi wanavyoweza kujiajiri kupitia utaalamu walioupata chuoni hapo.

“Nachukua fursa hii kuwapongeza vijana wote ambao wameweza kumaliza elimu yao, wamejituma vya kutosha na ndio maana wamehitimu masomo yao, kikubwa wanaenda duniani huko watakutana na changamoto zingine, ninachokisema ni kwamba wamepata masomo mazuri kwa hiyo wasitegemee kuajiliwa, wafikilie kujiajili

Wasifikilie kufanya kazi Tanzania pekee yake, kuna nafasi nyingi hasa ukanda huu wa Afrika mashariki, kwa hiyo wajikite Zaidi kutafuta fursa huko,” alisema

Sido inasaidia vijana, kwa hiyo hawa wanafunzi wanaweza kuwa sehehmu ya kuanzisha viwanda, tumeona hapa kuna mfano wa ndege nzurui tu imebuniwa, kwa hiyo tunahitaji vijana kama hawa kuwakuza ubunifu wao, wafungue viwanda kidogokidogo.

Sido tunatoa mafunzo ya ujasiliamali, mikopo kwa wafanyabiashara hasa wanaotaka kufungua viwanda lakini pia tunawaunganisha na wadau, kwa hiyo ujio wao katika shirika hili watapata ufumbuzi wa mambo mengi.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Prof Zacharia Mganilwa alisema chuo kimejipanga kuhakikisha kuwa idadi ya wataalamu wa anga kuendelea kuongozeka.

Alisema licha ya kwamba mafunzo hayo yana bei kubwa lakini wamejipanga kuona kadri mwaka unavyozidi kusonga mbele na idadi ya wanafunzi inaongezeka.

“Ni kweli tasinia ya anga tunao wahimu wachache, sababu kubwa ni haya mafunzo ni ghali, lakini niwahakikishie watanzania kuwa tunakuwa na wataalamu wa kutosha kuisaidia taifa.

 


No comments