Mkuranga wapata uongozi mpya wa soka
Na Kahema Juma Fimbo, Mkuranga
Hatimaye
chama cha soka Wilaya ya Mkuranga (MDFA) kimefanikiwa kupata safu mpya ya
uongozi wa soka ambao wanategemewa kuhudumu kwa kipindi cha miaka minne toka
Disemba, 2020 hadi Disemba 2024.
Akizungumza
mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi, Mwenyekiti mpya wa chama cha soka
Wilayani humo, Mwl Minael Njovu alisema uchaguzi ulikuwa na ushindani mkubwa
lakini ametoa shukrani kwa kufanyika kwa amani na washindi kupatikana.
Uchaguzi
huo ambao mara kadhaa uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali ulishuhudia
viongozi mbalimbali wakishinda nafasi zao walizoomba.
Nafasi
ambazo ziligombewa katika uchaguzi huo ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti,
Katibu Mkuu, mjumbe wa mkutano mkuu COREFA na mwakilishi wa vilabu.
Nafasi ya mweka hazina haikugombewa kutokana
na kukosa mgombea wa kugombea nafasi hiyo. Mkutano huo ulianza majira ya saa 4
asubuhi na uliiisha kwenye majira ya saa 7 mchana. Uchaguzi ulisimamiwa na
katibu wa kamati ya uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa pwani(COREFA) Ndugu
Masau Bwire.
Wajumbe
ambao waliruhusiwa kupiga kura katika mkutano huo walikuwa viongozi wa vilabu
vya soka katika wilaya ya mkuranga na viongozi wa chama cha marefa wilayani
mkuranga.wagombea wa nafasi hizo mbalimbali walipata nafasi ya kujinadi na
kutoa sera zao mbele ya wajumbe hao na wajumbe hao wakasikiliza na kisha kupewa
nafasi ya kuwauliza maswali wagombea hao. Wajumbe hao walipiga kura na hatimaye
kura zilihesabiwa katika majira ya saa 6 mchana. Baada ya kura kuhesabiwa
matokeo yalitangazwa na aliyekuwa katibu wa kamati ya uchaguzi Ndugu Paul
Nduru.
Wagombea
ambao walishinda katika uchaguzi huo ilikuwa Mwenyekiti alishinda mwalimu
Minael Njovu, makamu mwenyekiti Ndugu Kahema Fimbo, nafasi ya katibu mkuu
alishinda ndugu Bogras Bryson, nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa COREFA
alishinda ndugu mwalimu Denis Kalinga na nafasi ya mwakilishi wa vilabu
alishinda mwalimu Rajabu Tupa. Baada ya kutangazwa matokeo hayo mwenyekiti mpya
alipewa nafasi ya kuongea na kutoa neno la shukrani kwa niaba ya uongozi mpya
wa MDFA.

No comments
Post a Comment