MHE. LUKUVI APOKEA TAARIFA YA MGOGORO WA MATUMIZI YA ARDHI MTAA WA MTAKUJA KATA YA CHANG’OMBE JIJINI DODOMA
Na: Eliafile Solla
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na kamati
maalum iliyokuwa inashughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi Kata ya chang’ombe
jijini Dodoma leo Desemba 11,2020 ambapo amepokea taarifa kuhusu mgogoro huo.
Mgogoro
wa matumizi ya ardhi wa Mtakuja, Kata ya Chang’ombe katika eneo lenye hekta 10
umedumu kwa muda mrefu licha ya jitihada mbalimbali za Serikali za kuutafutia
ufumbuzi.
Serikali
iliunda kamati maalum ya kushughulikia mgogoro huo wa matumizi ya ardhi na
baadae kuamua kupanga na kupima eneo hilo na kubadilisha matumizi kutoka yale
ya awali na kuwa Makazi kutokana na uhalisia na maendelezo yaliyokwisha
kufanyika kupitia mradi wa maboresho wa mwaka 2015.
Kamati
hiyo imekutana na Mhe. Lukuvi jijini Dodoma leo na kuwasilisha taarifa na
mapendekezo yake jinsi ya kuushughulikia mgogoro huo ambapo Mhe. Waziri Lukuvi
atatoa maagizo baada ya kuipitia taarifa hiyo na kujiridhisha.
No comments
Post a Comment