TRL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA USAFIRI WA TRENI,SOMA HAPO KUJUA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wake John Pombe Magufuli, imeendelea kufanya jitihada ili kuimarisha suala la usafiri kwa wananchi wake ambapo imeshuhudiwa uwepo wa Magari ya Mwendo Kasi, Usafiri wa Treni kwa safari za Stesheni Pugu, Stesheni Mwakanga, halikadhalika uwepo wa Treni ya Kasi maarufu kama Deluxe, lakini Serikali kupitia Kampuni ya Reli Tanzania imeamua kuja na Mwarobaini mwingine wenye tija kwa wananchi.
Ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Focus Makoye Sahani ameeleza kuwa uongozi wa Kampuni
ya Reli Tanzania imeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida
kwenda bara, ambayo itaanza rasmi safari zake Jijini Dar es Salaam siku ya
Jumapili, Septemba 4, 2016 majira ya Saa tisa, huku akifafanua kuwa treni hiyo ya
huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa 12 kutoka Dar es Salaam ikiwa na mabehewa
8 ya daraja la 3, mawili ya daraja la pili yatakayo muwezeha abiria kupata
sehemu ya kulala, na mawili daraja la kwanza na katika stesheni za Morogoro na
Dodoma yataongezwa mabehewa mawili ya daraja la tatu.
Aidha ameeleza kuwa Treni ya Deluxe imebadilishwa
siku ya kuondoka badala ya Jumapili ambapo kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016
itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutokea kituo kikuu cha Dar es
Salaam, halikadhalika mabadiliko hayo yataongeza safari za treni ya kwenda
Mpanda kwa kutokea Tabora badala ya safari mbili kwa sasa zitakuwa tatu kwa
wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi.
Pia Kaimu huyo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL amesema
kampuni hiyo ya TRL imefanya uamuzi wa kihistoria wa kupeleka huduma za kuuzwa
tiketi za safari za Mjini Kasulu zitakazo anza Septemba Mosi, hivyo itafungua
kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kutoa huduma hiyo kwa wasafiri
wanaotoka Kasulu na Maeneo ya jirani,
Hivyo Kaimu huyo Mkurugenzi Mtendaji amewataka
wasafiri na wananchi kwa ujumla nchini, hususani kwa wale wa Mpanda na Kibondo
kutumia fursa ya kuongezwa safari na huduma kuletewa karibu kwa kufuata sheria,
taratibu na kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija ilyokusudiwa