LOWASSA AWEKEWA KIZINGITI NA POLISI MKOANI RUKWA,SOMA HAPO KUJUA

Msafara wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia
Chadema, Edward Lowassa umekwama kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi baada ya
polisi kuuzuia kwa hofu kwamba unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa anayetembelea mikoa hiyo.
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema
alianzia ziara yake mkoani Mbeya tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao
vya ndani katika majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake
mkoani Songwe wakati leo asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.
Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya
mikutano ya ndani Majimbo ya Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.
Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, Frank Mwaisumbe alisema kwamba polisi
walimpigia simu Lowassa juzi saa 1.00 jioni akiwa Tunduma wakimtaka
aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando
alipoulizwa kwa njia ya simu alisema waliwashauri viongozi wa Chadema
wapange siku nyingine ya ziara kwa sababu mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa