Wakati Benki ya CRDB ikiwa inasisitiza wateja wake kujitahidi kurejesha mikopo yao kwa wakati, idadi ya mauzo katika soko la hisa Dar es Salaam (DSE) imekua kwa asilimia 57 na kufikia shilingi bilioni 3.3 kutoka shilingi bilioni 2.1 wiki iliyopita kutokana na ukubwa wa idadi ya mauzo.
Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Mwandamizi wa Masoko DSE Mary Kinabo imesema idadi ya mauzo hayo yamekua kutokana na kupanda kwa idadi za hisa zilizouzwa kutoka shilingi milioni 1.6 hadi kufikia shilingi milioni 2.2.
Aidha Mary ameongeza kuwa Benki ya CRDB imeendelea kuongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa asilimia 49 ikifuatiwa na Soko la Hisa DSE ikiwa na asilimia 43 na ya tatu ni kampuni ya Bia nchini TBL yenye asilimia 4.
Mbali na hayo taarifa hiyo imeeleza kwamba licha ya mauzo kupanda lakini viashiria vya soko katika sekta ya viwanda vimeshuka kwa alama 19.47 baada ya bei za hisa.
MAUZO YA SOKO LA HISA YAZIDI KUPANDA,MERY KINABO ASEMA CHANZO,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:18:00
Rating: 5