Zinazobamba

TGNP YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUHUSU BAJETI YENYE MRENGO WA KIJINSIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi alipokuwa akifungua semina kwa waandishi wahabari kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia. Liundi alisema dhamira kubwa ya kukutana na wanahabari ni kutaka kujenga uelewa juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia pamoja na mahusiano yake katika jamii.


Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akifafanua jambo kwa wanasemina.

Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza kwa makini bajeti yenye mrengo wa kijinsia na maana yake.

Waandishi wa habari wakiwa katika vikundi kujadili kuhusu bajeti na jinsi inavyogusa kila mmoja wetu katika jamii. Wamiliki wa vyombo vya habari wameaswa kuanza kuwekeza katika mabaraza ya halimashauri kwani huko ndiko chimbuko la bajeti ya Dodoma.

Afisa mipango, uchambuzi na machapisho Bw. Deogratius Temba akiwasilisha mada kwa wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia. Temba amesema Bajeti yenye mrengo wa kijinsia haina maana kuwa bajeti inayolenga mambo ya wanawake badala yake ni bajeti yenye macho ya kuangalia makundi mbalimbali kwa kuyachambua.