Zinazobamba

MKURUGENZI TGNP AWAPA SOMO WAHARIRI, WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI,




Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari

SELEMANI MAGALI-DARESALAAM



Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi amewashauri wamiliki na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuanza kuwekeza katika habari za Mabaraza ya Halmashauri, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwatua ndoo kichwani wanawake walio wengi ambao kwa kiasi kikubwa wanaathirika na maamuzi yanayofanyika katika ngazi hiyo ya maamuzi.

Kitendo cha kuanza kuandika habari za mabaraza ya halmashauri kwa wingi kutasaidia kumurika changamoto mbalimbali zinazowakabili, jambo litakalosaidia kupata majawabu kutoka serikalini.
                          
Akizungumza katika semina maalum ya waandishi wa habari, Bi. Liundi amesema kwa muda mrefu habari za mabaraza ya Halmashauri zimekuwa sio kipaumbele kwa vyombo vingi vya habari, badala yakae wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kuwekeza katika bunge la Dodoma ili kupata habari.
Amesema kwa uzoefu ambao wameupata, wamegundua kuwa vikao vya madiwani ni sehemu muhimu kwa mustakabali wa maisha ya Mtanzania.
Nataka niseme hapa “ tasnia ya habari kwa ujumla wake tuwaombe waanze kuwekeza kwa kurusha habari za mabaraza ya Halmashauri, ifahamike kuwa lile ni bunge kama lilivyo la Dodoma, wakikosea pale basi kila kitu kinaharibika” Alisema.
Amesema masuala kama ya Maji, Afya, Zahanati, Shule na mengineyo mengi yanayopaswa kufikishwa katika kata, mitaa au vijiji  bajeti yake yote inafanyika Halmashauri, kukosa kiviripoti kunachangia kuendelea kudumaza hali za wananchi hususani Wanawake.
Aidha katika hatua nyingine, Liundi ametoa wito kwa jamii kuitumia dhana ya  utafiti wa uragabishi ili kuweza kuistua jamii kujitambua na kukua kimaendeleo
Bi. Liundi amesema utafiti wa Uraghabishi umesaidia kuleta mwamko katika Wilaya Saba ambazo wamezifanyia utafiti, kwani watu wengi wameweza kuchokozeka na kuanza kuhoji haki zao za msingi na hivyo kuongeza maendeleo katika kata zao.
Amesema katika utafiti wao walioufanya, katika wilaya za  Kisarawe, Kinondoni, Ilala, Morogoro, Tarime na Mbeya wameweza kufikia vikundi 222 , wanaume 1000 na wanawake 3000 na kugundua kuwa baada ya kufanya uragabishi kumekuwa na mabadiliko makubwa ya Kimaendeleo.
Aidha Kwa upande wake  afisa mipango, uchambuzi na machapisho  wa TGNP Bw. Deogratius Temba ameelezea dhana ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia kuwa ni bajeti yenye macho yanayogusa makundi yote ya Kibinadamu.
Alisema kama kuna dhana kuwa bajeti yenye mrengo wa kijinsia ni kutaka kuwapendelea wanawaake inapaswa kuondoka kwani si tafsiri sahihi ya bajeti hiyo
Akizungumzia Tafsiri sahihi ya bajeti hiyo, Temba alisema ni bajeti yenye uhalisia ambayo itazingatia mahitaji ya kimakundi na hatimaye kitaifa.