Zinazobamba

TRA YAZINDUA MPANGO KAPAMBE,NI WA KUBORESHA TAARIFA ZA MLIPA KODI,SOMA HAPO KUJUA


tr1
Pichani ni
Kamishna wa TRA Bw. Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TRA jengo la Milenium Makumbusho leo wakati akielezea kampeni ya kuhakiki namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN itakayoendelea mpaka mwezi wa kumi mwaka huu nchini kote, kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani Bw.Elaijah Mwandumbya.


MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) kupitia kwa Kamishina Mkuu wa Ofisi hiyo wamezindua zoezi maalumu kwaajili ya kuhakiki na kuboresha  taarifa za usajili  wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) .

Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo , Alphayo Kidata kwa kushirikiana na wafanyakazi wa ofisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es salaam, hivyo kuanzia sasa zoezi hilo litakuwa endelevu katika mikoa yote nchini ya bara na visiwani ,

Kidata alisema kuwa lengo kubwa la uzinduzi wa zoezi hilo ni kubadili mfumo wa sasa wa kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi kwa kuweka mfumo mpya unaoendana na ukuaji wa teknolojia ambao utakuwa na walipa kodi wake  wanaostahili kuwepo kwenye wigo.

Aidha aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia  kuwaondoa walipa kodi hewa ,kuongeza ufanisi  katika suala zima la usimamizi wa ukusanyaji  kodi kwa kiwango cha juu na kuwezesha ulipaji kodi  kuwa nafuu kwa mlipaji.

Hata hivyo katika hatua nyingine Kidata ametoa wito kwa yeyote mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi kufika  katika ofisi za mamlaka hiyo ili kuweza kupata utaratibu wa zoezi zima  jinsi linavyokwenda