NI KIINI MACHO TU DODOMA,NDOTO ZA JPM SASA KUGONGA MWAMBA,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI serikali ikijiandaa kuhamia Mkoa wa Dodoma,
Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa imebaini kuwepo kwa madudu
katika Sekretarieti ya mkoa huo, anaandika Dany Tibason.
Kamati hiyo imebaini kuwepo kwa
matumizi mabaya ya fedha za serikali ikiwa ni pamoja na kujiuzia magari ya
serikali bila kufuata utaratibu.
Japhet Hasunga, Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya
PAC ambaye ni Mbunge wa Vwawa (CCM) amesema, watumishi wamekuwa wakijiuzia
magari ya serikali, wakipeana pia wakiyatengeneza katika gereji bubu.
Mbali na hayo pia kuna sintofahamu kuhusu ujenzi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambao kamati hiyo imehoji sababu ya kununuliwa
kwa vifaa vipya wakati jengo halijakamilika.
Kutokana na kuwepo kwa madudu hayo katika
Sekretalieti ya Mkoa wa Dodoma, PAC imetoa maagizo saba kwa uongozi wa mkoa
kutokana na kushindwa kujibu hoja kutokana na Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali (CAG).
Hasunga ameagiza mambo saba; kwanza, kamati imeitaka
idara ya usimamizi wa mali za serikali kufanya uhakiki maalum wa mali za
serikali katika fungu 72 hasa magari yanayofanya kazi, yaliyoharibika na
yaliyouzwa na kuwasilisha taarifa ya uhakiki huo maalumu kwa kamati ndani ya
miezi mitatu.
Amemtaka Ofisa Masuhuri kusimamia kitengo cha
uhasibu ili kuzingatia viwango vya kimataifa ya utayarishaji wa mahesabu katika
utayarishaji wa mahesabu ya serikali ili kuepuka hati za ukaguzi zenye dosari.
Akitoa maagizo amesema, kamati inamwagiza Ofisa Masuhuri
kuzingatia sheria ya manunuzi ya mali ya umma na kanuni zake katika shughuli za
sekretalieti ikiwa ni pamoja na kupata vibari kwenye mamlaka husika
anapofanyika uhamisho wa fedha katika vifungu mbalimbali.
Mbali na hilo kamati imemuomba CAG kwa kushirikiana
idara ya mali za serikali kufanya tathimini ya kina kuiridhisha kamati iwapo
garama za Sh. 12.5 Mil zilizotumika katika ujenzi wa jengo la ofisi ya mkuu wa
mkoa kama zinakidhi thamani halisi ya sasa.
Hasunga pia ametoa agizo la tano kuwa Ofisa Masuhuri
awasilishe taarifa ya maandishi kuhusu matumizi ya kiasi cha Sh. 665.3 Mil na
chanzo cha fedha hizo kabla ya muda wa kazi kesho.
Ofisa huyo ametakiwa kuwasiliana na Ofisi ya Rais
Utumishi ili kuhakikisha nafasi za kazi zinazokaimiwa zinajazwa mapema iwezekanavyo
ili kuongeza ufanisi wa sekretalieti katika Mkoa wa Dodoma.
Agizo la saba lililotolewa na PAC kwa Mkoa wa Dodoma
amesema, kwa kuwa hoja nyingi za ukaguzi bado hazijapata majibu sahihi, kamati
kamati inatoa muda wa miezi sita kwa sekretarieti kukamilisho hoja za kukaguzi
na taarifa ya utekelezaji ziwasilishwe kwa CAG na kwa kamati kabla ya miezi
sita kuisha