MRITHI WA MAKONDA KINONDONI ATUMBUA JIPU,SASA AWA MBOGO,SOMA HAPO KUJUA
WALIMU wakuu wa shule 68 wa shule za Msingi
wanatakiwa kuvuliwa na kunyang'anywa vyeo vyao kwa kosa la udananyifu wa
takwimu za wanafunzi hewa tangu elimu itangazwe kuwa bure.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Ally Salum Hapi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo.
Amesema kuwa walimu wakuu hao wametakiwa kuvuliwa
vyeo vyao na kuwapa walimu wengine kwa kosa la kutoa takwimu za wanafunzi hewa
3462 wa shule za msingi 68 za Wilaya ya Kinondoni. Pia hatua kali za
Kisheria zitachukuliwa kwa dhidi ya walimu wakuu wa shule hizo.
Pia Hapi amemwomba Katibu Tawala wa Mkoa kuwavua
vyeo wakuu wa shule 22 wa shule za Sekondari 22 za Manispaa ya Kinondoni na
Ubungo kwa kosa la kutoa takwimu za uongo na kuweka wanafunzi hewa.
Wakuu wa shule za Msingi hao wamekuwa na wanafunzi
hewa 2534 kutoka shule 22 za Sekondari za Manispaa ya Kinondoni na
Manispaa ya Ubungo.
Wakuu wa shule hizo wameisababishia Serikali
kupoteza zaidi ya shilingi milioni 60 kwa kupeleka fedha za kuwahudumia
wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.
Baadhi ya shule za sekondari zilizokutwa na
wanafunzi hewa ni Boko wanafunzi 74, Bunju B155, Goba Mpakani 42 na Hananansifu
wanafunzi 154. Na shule za Sekondari ni Msisiri B wanafunzi hewa 395, Upendo
273 na Ubungo Msewe 267.