WAZIRI NDALICHAKO AVISHUKIA VYUO VIKUU AVITAKA KUREJESHA FEDHA HIZI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo
vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo, jijini
Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi
la uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo vyuo vya Elimu juu.
Prof. Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa
wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya vyuo 81 vilivyopo nchini.
Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.
Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.
“Mikopo ya Wanafunzi hao imesitishwa na
kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini walishindwa kujihakiki itabidi waombe
tena mkopo,” alifafanua Mhe. Ndalichako.
Ameendelea kwa kusema kuwa, kwa mwaka wa fedha
2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu Serikali kiasi cha shilingi 3,857,754,460.
Kutokana na mambo
yaliyobainika Serikali imechukua hatua zifuatazo
Vyuo vikuu ambavyo vimepokea fedha za wanafunzi
ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku saba kuanzia
August 17 2016
Vyuo vya elimu ya juu vinaagizwa kuweka mfumo mzuri
wa uhifadhi wa kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na
ya mitihani na namba za akaunti za benki ambapo fedha za mikopo hilipwa.
Vyuo vikuu vinaagizwa kuwasilisha bodi ya mikopo, kwa
wakati taarifa zote za kitaaluma na za kibenki za wanafunzi ili kuiwezesha
kufanya marekebisho stahiki katika kumbukumbu zao na kuepusha ulipaji wa fedha
kwa wanafunzi wasiostahili.
Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara
moja mabadiliko ya taarifa za wanafunzi kama zilivyopelekwa kutoka vyuoni ili
kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe na kuingiza mara
moja mabadiliko ya taarifa za waafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili
kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Vyuo viweke utaratibu mzuri wa kudhibiti malipo kwa
wanufaika wa mikopo ili kuepuka kufanya malipo kwa wanafunzi hewa.
Wakuu wa vyuo ‘VCs’ na Principals’ waweke mfumo wa
kuhakiki usahihi wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa bodi ya mikopo na
watawajibika kwa usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki
limebaini kuwepo kwa usdadanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi; wapo
ambao hawakufanya mtihani au waliofeli lakini wameandikiwa PASS ili waendelee
kupata mikopo.
Uchunguzi zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili
kubaini fedha za mikopo ambzo zimelipwa kwa watu wasiostahili. Hatua hii
inatokana na matokeo ya uchunguzi ambao umebaini kuwa wapo baadhi ya wanafunzi
waliohitimu tangu mwaka 2013 lakini wameendelea kupokea fedha na wengine
waliofukuzwa kwa kushindwa masomo tangu mwaka 2013/14 lakini bado wamelipwa
hadi mwaka 2015/16.