Zinazobamba

MZEE AKILIMALI AWAPIGIA "MAGOTI" WANA-YANGA, WENYEWE WASHINIKIZA AVULIWE UANACHAMA



Kufuatia taarifa ya kutuhumiwa na wanayanga juu ya kumtusi Mwenyekiti wa Klabu Yanga, Bw Yusuph Manji kuwa amekurupuka kuhusu kuomba ridhaa ya kukodishiwa klabu hiyo, Leo Mzee Akilimali ameibuka na Kuwaomba radhi mashabiki na familia nzima ya wana-yanga akisema haikuwa dhamira yake kumtukana na kwamba ni jambo ambalo linamnyima usingizi toka alipolitamka.

Mzee Akilimali amesema anaomba msamaha kwa kitendo hicho, na anaamini kuwa wanayanga watamuelewa kwani si nia ya mwanayanga yeyote kuharibu umoja na mshikamano uliopo.

"Kwa kweli Sijamtusi mwenyekiti wangu kwa kusema amekurupuka. Neno hilo ni la kawaida wala sikuwa na dhamira ya kumtusi mwenyekiti wangu, nawaomba radhi wana-Yanga kwa kauli zangu. Usiku sijalala nilikosa raha mara baada ya kusikia Manji kajiuzulu" Alisema Mzee akilimali.
Mie naomba tuwe na umoja tatizo letu na mwenyekiti ni kushindwa kutuita wazee kwenye mpango wake wa kuichukua timu. 
Sisi tunampenda na kumuhitaji sana Yusuf lakini tunahitaji aendeleze mfumo wa zamani alioanza nao wa kujali na kuthamini wazee ili nasi tujisikie vizuri na klabu yetu. 
Nasisitiza sina chuki na Manji maana kwa mdomo wangu huu nimeshiriki sana kumuweka madarakani mpaka pale umma wa watanzania wakasema tumevunja katiba. Ninachotaka alitambue Baraza la Wazee na sisi tukae nae tuzungumze mstakabali wa klabu yetu.

Katika hatua nyingine Viongozi wa  matawi wa klabu ya Yanga leo saa nne walikutana katika kikao cha dharura kufuatia mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu na kutupilia mbali mpango wake wa kutaka kuikodisha timu hiyo na kuiendesha kibiashara kwa miaka 10.

  Taarifa za Manj  kujiuzulu zilikuja kufuatia tuhuma kuwa kuna baaadhi ya viongozi wa Yanga wamemkashifu na mmoja aliyetuhumiwa kwa kosa hilo ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee, Yahya Akilimali.

Katika kikao cha leo, Viongozi hao wa Matawi wamefikia maazimio haya, lengo likiwa ni kuleta mshikamano na umoja klabuni hapo.


  •   Viongozi wa Matawi wamemtaka Katibu Mkuu wa Yanga kumfuta uanachama wa Yanga Yahya Akilimali kwa kosa la kumkashifu mwenyekiti wa Yanga.
  • Viongozi hao wamelaani taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Wazee, Mzee Akilimali na kuwa haikuwa taarifa iliyopewa baraka na Yanga.
  •   Katiba ya Yanga hailitambui Baraza la Wazee badala yake inalitambua Baraza la Wadhamini, hivyo basi viongozi wa Yanga wamemuomba Katibu Mkuu wa Yanga kuvunja Baraza la Wazee na wazee hao warudishwe katika matawi wawe wanachama wa kawaida.

  • Mwanachama yeyote wa Yanga atakayeongea na vyombo vya habari bila idhini ya Yanga, atakuwa amejifuta uanachama wake.