Zinazobamba

RC MAKONDA AIBUKA NA HIKI LEO,SASA AJITOSA KUWAJENGEA JENGO BAKWATA,SOMA HAPO KUJUA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtJkn9ZTV05CfquY4_TvyAXzfFzI88Cb-WoqGDhWKqkDpUbH-DXZuT9KzdBuvwBgTLJ5jJJ9fRtHz6oib80eV0wNPn4abj65-TdRRN0AHFs1UibAKRmcoEqR3JRgZFE9fIsxeUWEd3zMc/s1600/OTH_7724.JPG
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir wakitazama mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu,ambapo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tano,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum .


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo. 

Pamoja na kukabidhi ramani hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema jengo hilo litagharimu kiasi cha fedha 5, 080, 155, 600 ili kukamilika.
Pia amesema jengo hilo mpaka kukamilika litakuwa la kipee na kupewa hadhi kama  Taasisi kubwa ya Kiislamu na kusisitiza ujenzi wa jengo hilo hautazidi miezi 14.

Amesema amekabidhi mchoro huo kutokana na kutambua na
kuthamini umuhimu wa BAKWATA katika Taifa pamoja na kuwataka Waislamu na wasiokuwa waislamu kujitokeza katika kutoa misaada hiyo.
Pia ametoa shukrani kwa waislamu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushereheka nao  pamoja katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo amesema mwezi
huo ndio uliokuwa chimbumbo la ujenzi wa jengo hilo la BAKWATA.

Akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti  Abuubakari Zuberi amewataka Waislamu kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa huyo ikiwa kuwataka kuamini ya kuwa na haki ya kupokea misaada kama Waislamu.