BENKI YA EXIM YASHEREKEA MIAKA 19 NA KUIBUKA NA KITU HIKI,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
|
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani
Mponda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kabla
ya hafla fupi ya kusherekea miaka 19 ya benki hiyo na kuzindua wa huduma tatu
za benki hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha cha Hatari katika Benki ya Exim Bank,David Lusala. kulia ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick
Kanga
|
BENKI ya Exim Tanzania imesheherekea kuadhimisha
miaka 19 ya ukuaji na uvumbuzi kwa kuzindua huduma mpya tatu kwa wateja wake
jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda amesema
kuwa leo wanasherekea miaka 19 tangu kuwepo hapa nchini ikiwa na mafanikio
makubwa Katika miaka 19, benki hiyo imejenga utendaji bora na imara
katika fedha wakiwa na rasilimali zenye thamani ya TZS 1.5 Trilioni kufikia
Juni 2016.
Amesema kuwa Faida kabla ya kodi katika kipindi cha
pili cha mwaka ilikuwa shilingi bilioni 64 na pia wameweza kuwa na wastani wa
ukuaji kwa mwaka wa asilimia 30.
Mafanikio ya benki ya Exim Tanzania ni kuweza kuwa
na makao nchini Uganda kwa kununua benki ya Imperial ya Uganda mapema mwaka
huu. Benki ya Exim sasa ina hisa za asilimia 58.60 katika taasisi hiyo mpya
ambayo inayofanya biashara kama Benki ya Exim Uganda. Wakati ikijikita kuwa
benki ya kikanda tayari ina matawi 43 katika nchi nne zikiwemo Tanzania,
Uganda, Djibouti na Comoro na pia ikiwa na mipango ya kuendelea kujitanua
katika masoko mengine katika miaka mitano ijayo.
Amesema kuwa huduma zilizozinduliwa ni:-
1. Uwezo wa kutoa taarifa za udanganyifu katika
kampeni ya kupambana na udanganyifu ikiwa na lengo la kutengeneza mazingira ya
kutokuwa na wizi katika tasnia ya benki.
2. Kadi za malipo za Exim (TANAPA cards,
Master cards and VISA cards) ambazo zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za
Taifa chini ya TANAPA. Kadi hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki
na pia kuzuia upotevu wa mapato katika tasnia ya Utalii.
3. Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao
unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi
kikubwa.
Katika miongo miwili iliyopita, ukuaji wa benki hii
na mchango wake wa kiuc humi na kijamii umetambulika sio tu katika Tanzania
bali pia katika kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa sababu ya ubora
katika utendaji wake.
