Zinazobamba

MBUNGE KUBENEA AANZA KULITIKISA BARAZA LA MAWAZIRI JPM,WAZIRI WAKE AIBUKA NA KULIA NA GAZETI LAKE,SOMA HAPO KUJUA



 Saed Kubenea, Mbunge wa jimbo la Ubungo
NA KAROLI VINSENT
MBUNGE wa Ubungo,Saed Kubenea ambaye ni Mmiliki wa Kampuni ya Hali halisi Puplish ambao ni wachapishaji wa Gazeti la Mwanahalisi na Mseto  teyari kwa sasa ameanza kulitikisa baraza la Mawaziri la Rais John Magufuli ndivyo naweza kusema baada Mmoja wa mawaziri wa Magufuli kuibuka na kutaka alipwe bilioni 1 na kampuni hiyo kwa madai kuwa amechafuliwa.

Anayetaka malipo hayo ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawaliano,Mhandisi Edwin Ngonyani amedai kuwa atamfikisha Mahakamani Mmiliki wa Gazeti la Mseto ambaye ni Kubenea,Mwandishi wa Gazeti hilo,Josephat Isango pamoja na Mchapajishaji wa Gazeti hilo kutokana na kuandika habari anayodai imechafua.

Mhandisi Ngonyani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Natumbu ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari, amesema Gazeti la Mseto la Alhamisi ya tarehe 4 mwezi huu Gazeti hilo lilibeba kichwa cha habari “Waziri wa amchafua JPM”


Amedai habari hiyo iliyochapishwa ukrasa wa mbele huku ikiweka picha yake pamoja na picha ya Rais John Magufuli huku taarifa hiyo ikimtaja Mhandisi Ngonyani kuwa wakati alipokuwa mkurugenzi wa Stamico alipokea fedha  toka wafanyabiasha zilizodaiwa kumsaidia mpaka kuwa mbunge na baadaye kufanikiwa kuwa Naibu Waziri.

Amejitetea kuwa Habari hiyo ni ya uongo yenye lengo la kumchafua yeye kwa jamii pamoja kuweka nia hovyo kwa Rais Magufuli kuwa alisaidiwa na wafanyabiasha mpaka kupata madaraka ambapo Rais Magufuli kila mara amekuwa akipinga kuwa yeye hakusaidiwa na mfanyabiashara.

Mhandisi huyo ameenda mbali na kudai kuwa hata (Document) iliyochapishwa ukrasa wa mbele ambayo mwandishi wa habari hiyo,Isango ameitumia kama chanzo cha habari ni ya kufoji kwani hata tarehe iliyoandikwa wakati yeye akisaini barua hiyo alikuwa teyari ameacha kazi.

Amesema baada ya kusoma habari hiyo na kujilizisha siyo ya ukweli ameliandikia baraua gazeti hilo ndani ya siku saba kumuomba radhi kwa uzito ule ule habari ilivyoandikwa na kutoa fidia bilioni 1 kwa kile anachodai kuchafuliwa hadhi yake,
Amesema endapo Gazeti hilo likikataa kufanya hivyo,basi atamfikisha mmiliki wa Gazeti hilo,Mwandishi wa Habari hiyo,Josephat Isango pamoja na mchapishaji wake mahakamani ili hatua zaidi zichukuliwa.
     WADAU WANENA.
Wakizungumzia hali wadau mbali mbali wa masuala ya habari wamesema hatua ya Mhandisi Ngonyani inaweza ikawa ya kutisha kwa sababu  kuwa viongozi wengi hawaitekelezi.
“Ujue Yule mwandishi Isango hawezi akaandika habari ile kwa kutunga,ni jambo la kutafakali tu hivi tangu viongozi hawa waandikwe  kwenye magazeti ni mara ngapi wanakuja na matamko na vitisho kama hivi na wanaishia kuwa kimya, “amehoji mwandishi mmoja wa Gazeti linalotoka kwa siku.